BURUDANI: CHIDI BENZ ANUSURIKA KIPIGO NA MASHABIKI AKIPERFORM CLUB MAISHA DODOMA, WADAI ANAUCHIZI

Msanii wa hiphop nchini Chidi Benz alinusurika kupigwa na mashabiki wake mjini Dodoma alipokuwa akifanya show New Maisha Club.
Kitendo hicho kilikuja baada ya msanii huyo kutoa Bangi mfukoni mwake na kuiwasha ili avute ndopo mashabiki walipopiga kulele za kuashiria ni utovu wa nidhamu kwani hata Jamhuri hairusu kitendo hicho.
Hata hivyo Baunsa wa maisha club aliwahi kumpokonya bangi hiyo kabla haijasababisha kero zaidi. Baadhi ya mashabiki waliokuwa humo ndani walisikika wakimuita "CHIZI BEZ" wakiashiria kuwa ni mgonjwa wa akili na baadhi walipiga makelele "Wa Mirembe huyo!!"
Kitendo hicho kimemshushia hadhi msanii huyo wa Ilala na kumfanya aonekane kama msanii asiyekuwa na mipaka ya kimaadili.