jaridahuru

Mitandao

AFYA: BINTI WA KIMASAI, SELITIAN NATA, ANAESUMBULIWA NA UVIMBE MGUUNI AOMBA MSAADA WA MATIBABU

Na John Gagarini, Bagamoyo.
 
MSICHANA Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo kata ya Vigwaza Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani yuko kwenye hali mbaya ya kiafya baada ya kuvimba mguu na kuwa kwenye maumivu makali.Ugonjwa huo uvimbe huo ulianza kama kipele kidogo miaka zaidi ya 10  iliyopita lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda ndipo uvimbe huo ulizidi kuongezeka na kufikia usawa wa mbavu.
 
Akizungumza na waandishiw ahabari ambao walimtembelea nyumbani kwao alisema kuwa uvimbe huo una ambatana na maumivu makali pamoja na homa kali hasa nyakati za usiku.
 
“Niko kwenye wakati mgumu kama mnavyoniona napata shida naomba nisaidiwe kwani nimekwenda hospitali toka kipindi hicho lakini sikupata matibabu zaidi ya kupewa vidonge tu ambavyo hupunguza maumivu lakini uvimbe uko pale pale,” alisema Nata.

Nata ambaye ana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (2) alisema kuwa wakati tatizo hilo linaanza alikwenda hospitali mbalimbali lakini hakuweza kupatiwa matibabu sahihi na kupelekea uvimbe huo kuongezeka hadi hapo ulipofikia na kumkosesha raha.
 
“Naomba wataalamu mbalimbali pamoja na wafadhili ili niweze kupata matibabu sahihi ambayo yataondoa uvimbe huu ili name niweze kuishi kwa raha kama wengine,” alisema Nata.
 
Kwa upande wa baba yake Nata Mumbi alisema kuwa alimpeleka mwanae kwenye hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu lakini hakuna mafanikio yoyote.“Tatizo matibabu ambayo wanayompa si ya kina jambo ambalo linasababisha mwanangu asipate nafuu, lakini kupitia vyombo vya habari naomba wasamaria wema wamsaidie mwanangu ili aweze kupata matibabu sahihi,” alisema Mumbi.
 
Aidha alisema kuwa anashangaa kuona kila anapokwenda hospitali mwanae anapewa vidonge tu jambo ambalo linafanya wakate tamaa ya kumpatia matibabu. 

Related

JAMII: MZINDAKAYA AONJA CHUNGU YA MAGUFULI, ANYANG'ANYWA NYUMBA 12 NA WIZARA YA UJENZI

WIZARA ya Ujenzi imeinyang’anya Kampuni ya Agriculture and Animal Food Industries Ltd (Saafi), inayomilikiwa na mwekezaji mzalendo na mwanasiasa mkongwe, Dk. Chrisant Mzindakaya nyumba 12 za umm...

AJALI: DEREVA APONA KUTOKA KWENYE AJALI MBAYA BAADA YA GARI LAO KUANGUKIWA NA KONTENA ATOKA MZIMA

This is the incredible moment two people were pulled alive from a car that had been almost entirely flattened by a shipping container falling on top of it. Firefighters arriving at the scene in Qin...

AFYA: EBOLA YAZIDI KUINYEMELEA AFRIKA MASHARIKI, FAHAMU JINSI YA KUJIKINGA NA EBOLA NA MADHARA YAKE

Mgonjwa wa EBOLA Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na kirusi kiitwacho ebola. Kirusi hicho ni moja kati ya familia ya virusi watatu toka katika familia ya filoviridiae. ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item