jaridahuru

Mitandao

KIMATAIFA: WATU 157 WAFA KATIKA MGODI WA MAKAA YA MAWE UTURUKI



Mlipuko katika mgodi wa makaa ya mawe magharibi mwa Uturuki umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji migodi 150 na kujeruhi wengine zaidi ya 70 kwa mujibu wa maafisa nchini humo.
Meya wa eneo la Manisa, Cengiz Ergun, ametoa tahadhari kwamba idadi ya watu waliokufa bado haijathibitishwa rasmi.

Inahofiwa kuwa wachimbaji mgodi wengine wengi bado wamefukiwa chini ya mgodi huo.
Inakadiriwa kuwa wakati mlipuko huo ulipotokea wafanyikazi 580 walikuwa ndani ya mgodi huo japo inaaminika wengi waliweza kukimbilia usalama wao .Bado idadi ya walionaswa ndani ya mgodi huo haijabainika. 

Mgodi huo uko katika mji wa Soma, mkoani Manisa , takriban kilomita 250 kusini mwa Istanbul.

Jamaa za wachimbaji migodi hao wamekusanyika katika makundi karibu na mgodi huo ambao unamilikiwa na wawekezaji wa kibinafsi huku wengi wao wakilia hadharani na kububujikwa na machozi.

Waziri wa nishati Taner Yildiz ameimabia televisheni ya Uturuki kuwa huenda wengi wamekufa kutokana na sumu ya gesi aina ya carbon monoxide.

Amesema moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme.
Picha za televisheni zinaonyesha maafisa wa uokoaji wakiokoa wafanyikazi wa mgodi huo, huku nyuso zao zao zikiwa zimejaa vumbi.
Baadhi yao wanaweza kutembea na wengine wanabebwa na kupelekwa ndani ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyoegezwa karibu na eneo la tukio.

Chanzo: BBC

Related

KIMATAIFA: BOKO HARAM WABADILISHA NIA KWA WASICHANA, WAKATAA KUWAACHIA KWA HOFU YA KUKAMATWA

Kiongozi mmoja wa kanisa la kianglikana anayehusika katika majadiliano ya kuwaachilia huru mamia ya wasichana waliotekwa nyara nchini Nigeria amesema kuwa wengi wao wanazuiliwa nje ya taifa hi...

KIMATAIFA: JAMHURI YA AFRICA YA KATI YAPIGA MARUFUKU 'SMS', HAIRUHUSIWI KUTUMA AU KUPOKEA UJUMBE WA SMS

  Wakati Tanzania kukiwa na kampeni ya kukomesha tabia za kusambaza ujumbe mbaya kwa simu ya mkononi au mtandaoni tuliyoipa jina la ‘Delete Futa Kabisa’, serikali ya Jamhuri ya Afrika Maghari...

KIMATAIFA: WANNE JELA KWA KUFANYA MAPENZI YA JINSIA MOJA , LICHA YA SHERIA KUTOWEKA WAZI KOSA HILO - MISRI

Mahakama moja nchini Misri imewahukumu watu wanne kifungo cha hadi miaka minane jela kwa kosa la vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja. Watu hao wanashutumiwa kuhu...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item