jaridahuru

Mitandao

KIMATAIFA: SUDANI KUSINI WAKIUKA SAINI YA MAKUBALIANO YA AMANI WAINGIA VITANI TENA


Saa chache tu baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa usitishaji mapigano nchini Sudan kusini Malumbano yameibuka .

Sasa Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini wanalaumiana kila upande ukimshutumu mwenzake kuvunja makubaliano hayo yaliyosainiwa ijumaa.

Hata hivyo kiongozi wa waasi Riek Machar anasema bado ameazimia kutekeleza makubaliano hayo licha ya kwamba anasema serikali ya rais Salva Kiir inavunja mapatano hayo.

Machar amesema kuwa majeshi ya UPDF ya Uganda ambayo yamekuwa yakivamia maeneo inayoyadhibiti haijaafiki mkataba uliotiwa sahihi huko Adiss Ababa kati yake na Rais Salva Kiir.
Aidha msemaji wa jeshi la serikali, Kanali Philip Aguer, amesema waasi hao wameshambulia maeneo ya serikali katika mji wa Bentiu .

Upinzani umepinga madai hayo.
Machar amesema kuwa angetaka mazungumzo zaidi na serikali kuhusu hilo, lakini amesema anafahamu kuwa Rais hana uwezo wa kudhibiti majeshi yote yanayopigana kwa upande mmoja na majeshi ya serikali kama vile majeshi ya Uganda na wapiganaji kutoka Darfur.
Serikali ya Sudan Kusini pia imelaumu upande wa waasi kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano saa chache tuu baada ya mkataba huo kutiwa saini.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Ijumaa, na yalikusudiwa kumaliza vita vya miezi mitano ambavyo vimeuwa maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni moja kuhama makwao.

Chanzo: BBC

Related

KIMATAIFA: MIGOMO AFRIKA KUSINI YASABABISHA KUDUMAA KWA UCHUMI

Mazungumzo yaliyonuiwa kumaliza mgomo katika sekta ya madini Afrika kusini yamesambaratika. Waziri wa maswala ya madini nchi humo ,Ngoako Ramatlhodi, amesema juhudi zote za kupatanisha wenye mak...

KIMATAIFA: KIONGOZI WA KUNDI LA MUNGIKI KENYA 'MAINA NJENGA' AMESHAMBULIWA KWA RISASI

NYAHURURU, Kenya. Aliyekuwa Kiongozi wa kundi la Mungiki lilowauwa na kuwachinja wananchi wa Kenya katika vurugu za baada ya uchaguzi Kenya, Maina Njenga, ameshambuliwa kwa risasi huko Kenya. Njen...

KIMATAIFA: HERMAIN KATANGA WA KONGO AHUKUMIWA JELA MIAKA 12 NA MAHAKAMA YA ICC

Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imemhukumu kiongozi wa zamanai wa wanamgambo waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Germain Katanga, kifungo cha miaka kumi na miwili jela baada ya kum...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item