jaridahuru

Mitandao

JAMII: MAMA MZAZI WA ZITTO KABWE HOI ICU, ASHINDWA KUHUDHURIA BUNGE LA BAJETI

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (Chawata), Shida Salum, yuko katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani.

Shida ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amelazwa tangu juzi. Alianza kusumbuliwa na maradhi hayo mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu akiwa mjini Dodoma akisubiri kuapishwa pamoja na wajumbe wengine wa Bunge Maalumu la Katiba.

Akizungumza hospitalini hapo jana, Zitto alisema baada ya hali ya mama yake kuwa mbaya alishindwa kuendelea kukaa Dodoma kusubiri kuapishwa na alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako aligundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na kupatiwa tiba kwa mwezi mmoja kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

Alisema kabla ya kupelekwa hospitalini hapo, alikuwa akiendelea kupata matibabu akiwa nyumbani, lakini hali yake ilibadilika juzi.
Zitto alisema hali ya mama yake haijatengemaa tangu aanze kusumbuliwa na maradhi hayo. Alisema kutokana na maradhi hayo ya mama yake, ameshindwa kuhudhuria Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.

“Hali ya mama kwa kweli siyo nzuri, lakini nina imani itakuwa nzuri na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa kama zamani,” alisema Kabwe.
Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Zitto alionekana Dodoma mara moja tu, siku ilipowasilishwa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Related

AFYA: BINTI WA KIMASAI, SELITIAN NATA, ANAESUMBULIWA NA UVIMBE MGUUNI AOMBA MSAADA WA MATIBABU

Na John Gagarini, Bagamoyo.   MSICHANA Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo kata ya Vigwaza Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani yuko kwenye hali mbaya ya kiafya baada ya kuvimba ...

JAMII: SIRI NZITO BIDHAA ZA MACHINGA, WATAKIWA KULIPA FAINI YA 400,000

Kilichotokea mnadani Katika eneo la mnada wa kuuza vitu vya machinga vilivyokamatwa lililopo katika Soko la Kibasila Gerezani, kulikuwa na makundi ya watu wa ...

JAMII: ASKOFU AWATAKA WATANZANIA KUTOKUBALI KUGOMBANISHWA NA WANASIASA WACHOCHEZI

  Watanzania wametakiwa kutokubali kugombanishwa na wanasiasa  ambapo hivi sasa kumekuwepo na siasa navyama vingi ili kuepuka kuleta vurugu na kuvunja amani ambayo nchi ya Tanzania im...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item