VYUONI: UCHAFU WANAOFANYA WADADA VYUONI, JE WAZAZI WANAWAFAHAMU BINTI ZAO?

Katika siku za hivi karibuniwanafunzi hasa wa vyuo vikuu wamekuwa na tabia chafu ya kujirekodi wakiwawanafanya mapenzi, na kupiga picha za utupu nakuziweka katika mitandao ya kijamiii.

Juzi tu, Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma wamekuwa na skendo za kujiuza kwa waheshimiwa wabunge, sio hao tu,wanafunzi wa chuo Cha Elimu ya Biashara wamerekodi mkanda wa ngono, Chuo cha Mipango nao haya, IFM nao wanapiga picha za utupu na kuweka kwenye mitandao.
Kwa kweli hii ni aibu kubwa kwa taifa linalowategemea wasomi hawa, inawezekana huko baadae kukawa na uhalili sasa wa kufanyahata ngono katika hadhara.
Kwa upande wa wazazi, ni ukweli usio pingika kuwa wengi wa wasichana hawa wa vyuo hutoka majumbani kwao kuja kusoma wakiwa na tabia njema lakini hubadilika punde tu wanapokutana na wasichana walio shindikana makwao.
Wazazi pia walalo jukumu la kuongea na binti zao ili kuwapa elimu dunia, kwani haya wanayoyafanya hupelekea wengi wao kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI na mwisho wake kushindwa kuendelea na masomo.
Serikali pia iangalie, na kutilia mkazo katika vyuo hizi, ili anayebainika kuwa na tabia za namna hii achukuliwe hatua na kisheria na jamhuri pia nakupewa adhabu ya chuo ikiwezekana kufukuzwa kabisa chuo.

