jaridahuru

Mitandao

JAMII: KATIKA KILE KINACHODAIWA KUWA KULIPIZA KISASI, ASKARI POLISI WAFUKUZWA NYUMBA ZA KUPANGA URAIANI


WAKATI Jamii ikiendelea kulia na vitendo vya Jeshi la Polisi nchini Tanzania, kila kukicha bila serikali kutoa tamko lolote juu ya manyanyaso hayo, Askari hao wenye dhamana ya kuwalinda raia na mali zao wameanza kuonja joto la jiwe. Askari Polisi nchini Tanzania wanaoishi uraiani katika nyumba za kupanga za raia wameanza kufukuzwa kwenye nyumba hizo huku raia hao wakianza kujipanga namna ya kuwanyika Askari hao huduma muhimu kama maji, na mahitaji mengine madukani.
Hivi ndivyo hali ilivyo nchini Tanzania
Raia nchini Tanzania wameanza kuchukua hatua hiyo baada ya kuona ndugu,jamaa na marafiki zao wakipata vipigo kiasi cha kupoteza uhai nawengine kupata ulemavu wa kudumu bila huruma, kwa maelezo kwamba wametumwa na viongozi wao wa ngazi ya juu wafanye hivyo.
Katika mtandao wa Jamii Forums kumekuwa na mada tangu jana kuhusu namna Polisi wanavyo nyanyasa raia na hatua ambazo raia wameanza kuzichukua dhidi ya Askari hao, hatua hii imekuja wiki moja tangu Tovuti ya Habarimpya.com unayoisoma hivi sasa, ilipoanza kampeni ya kukemea matukio ya Jeshi la Polisi kuwapiga raia wema, Habarimpya.com imekuwa ikilaani tabia hiyo ya Jeshi la Polisi kwa kuandika makala mbalimbali na picha katika Ukurasa wake wa Picha.
Rai mmoja Askari watatu, je hapa kuna haki za binadamu?
Topic: Nimewafukuza Polisi waliopanga kwenye nyumba yangu Nimefanya maamuzi hayo huku nikiwa na akili timamu , Nimewataka kesho waondoke wakatafute nyumba nyingine za watu watakao kubaliana na uharamia wanaoufanya wa kupiga watu wasio na hatia. Kimsingi polisi hao watano ambao wameanza kazi miaka si mingi nawadai pango la miezi mitatu ya nyuma nimewaambia waende nazo sizihitaji. Siwezi kukaa na nyoka ndani ya nyumba ambao kila siku wanasababisha vilema kwa watu.
Waende wakapange nyumba za wanaCCM wenzao. Mara ya mwanzo wakati wenzangu wanalalamika juu ya polisi kuwapa vilema ndugu zao niliona kama
mchezo , lakini kitendo cha watoto wa ndugu yangu kuathirika na vipigo vya polisi jana imeniuma sana. Hawa polisi si watu wakuwachekea hata kidogo, ni
watu wasiofaa kabisa katika jamii , ni watu wa kuwatenga Ukiwauliza kwa nini mnafanya hivyo utasikia tunatumwa, kwa nini wasikatae? Mbona
polisi wa Nigeria walikataa kwenda kulinda maeneo ya Bokoharamu? Tumewachekea sana lakini sasa inatosha , mkakae kwenye vibanda vyenu vya mkoloni.
Polisi wanavyo tekeleza kauli ya Waziri Mkuu Pinda kwa vitendo.
Watu wenyewe maskini huku mitaani tunawalisha , tunawanywesha, tunawapa na malazi na wake zenu tunawaruhusu kuchota maji bure katika visima vyetu lakini bado hamna shukrani . Hakikwanza 22:13 Yesterday Good start, thank you Aisee hyo kali mdau Hongera mkuu na mimi nawakataza polisi kuchota
maji kwenye bomba langu la maji ya kisima kirefu. Waende kuchota huko huko juu wanakopokea amri. Shime watanzania wote tusiwape polisi ushirikiano
wa kijamii popote pale walipo nchini Tanzania.
Umefanya jambo la msingi sana mkuu ,waende wakaishi kwenye mabanda yao ya kufugia Kuku.Kuwatenga ni ujumbe tosha Hao jamaa nasikia hata daladala wanapanda bure lakini kumbe ni watu wenye roho mbaya kuliko wanyama. Nimemsikia Ofisa wa CUF aitwaye Kambaya aliyeumizwa kichwani akizungumza ITV na kusema kapigwa na Polisi ambaye anamfahamu kuwa ni msaidizi wa RPC Temeke tena kwa kutumia Tyre lever ya gari. Sasa hao watu wa aina hiyo ni wa kuwapangisha nyumba yako? Hata mie kama ningekuwa muuza duka siwauzii hata waje na hela.
Mimi nimepingua urafiki na polisi wawili,jana wamenikuta bar wakadhani nitawapa ofa ya bia kama kawa,niliwatazama tu..si unajua walivyopigika
hawa washikaji Kuanzia leo naweka bango linalosema "NYUMBA HII HAIPANGISHWI KWA POLISI YEYOTE" Kesho mbona Mbali watoke hata sasa hivi Magaidi
hao

Related

Jamii 5199693109587227748

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item