BURUDANI: USUPASTAA KWELI KAZI!! CHEKI KIVAZI CHA LULU KILICHOZUA GUMZO MTANDAONI

https://jaridahuru.blogspot.com/2015/02/burudani-usupastaa-kweli-kazi-cheki.html
Hakuna anaebisha kuwa mrembo na mwigizaji wa filamu Diana Elizabeth Michael ‘Lulu’ni moja kati ya mastaa wanaokwenda na fasheni na huwa hakosei kwenye hili, yaani huwa yupo “on point”.
Picha za mwanadada Lulu akiwa amevalia kivazi ambacho kwa kiasi kikubwa kimemuacha miguu yake wazi zilisambaa kwa kasi sana mtandao hapo jana, hii ni kutokana na watu wengi kuzi LIKE na ku-SHARE.
Kama kawaida yetu wa bantu, japokuwa wengi walitupia COMMENTS za kumsifia wengine pia waliponda uvaaji wa kanguo hako, na wengine kuanza kumtio kasoro, mbali na yeye mwenye Lulu kuandika mamaneno haya kwenye moja kati ya picha hizo.
“Sema nini.....tumiguu twangu tumenyooka hatuna kona...chaiiiii.. Na tumatege flani amaizing …Usinipanikie Mimi Lakini”by Lulu.
Kwa mtazamo wangu kwanza kabisa ni ukweli Lulu DIVA waukweli hapa mjini, sasa hilo swala la mavazi gani ndio ya maadili nawaachia nyie, mnalionaje hapa
Jionee picha hizo akiwa na kavazi hako hapo juu