jaridahuru

Mitandao

SIASA: UTABIRI WA RAIS AJAE WACHUKUA SURA MPYA, ASKOFU MOKIWA NAE ATAJA MAONO YA NANI ATAKUWA RAIS 2015

Askofu Mokiwa akisalimiana na Mhe, Mizengo Pinda

WAKATI Tanzania ikitarajia kufanya Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa amewataka watanzania kutochagua Rais ajaye kwa kuangalia sura yake.

Badala yake, awe ni kiongozi bora, atakayeweka mahitaji ya nchi mbele na atakayepimwa kwa utayari na uwezo wake.

Aidha, amewataka watanzania kuangalia chama kitakachosema ukweli na kitakachohamasisha na kujenga amani; na siyo kitakachochochea uvunjifu wa amani.

Mokiwa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kuzungumzia uzinduzi wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Dayosisi hiyo.

“Mpaka sasa mimi sina uso wa fulani kwamba ndiye atakuwa Rais, ila ninawaasa watanzania kuchagua kiongozi bora ambaye ataweka mahitaji ya nchi mbele, ikiwemo suala la afya na elimu,” alisema na kuongeza: “Tumekuwa tukisikia fulani kapelekwa India kutibiwa au Afrika Kusini, sasa kwa nini hao wataalamu wasiletwe hapa nchini kutoa huduma hizo?

Sisi tunaamini kwamba kanisa lenye wagonjwa ni lisilo na matumaini na lenye matumaini ni la wenye afya bora, vivyo hivyo na kwa serikali pia.

“Tusiweke uso wa mtu pale, tuangalie nani atakayefaa katika hayo na kuhakikisha anasimamia sera za afya zisihujumiwe. Pia elimu nayo iboreshwe maana kuna changamoto nyingi hivyo zishughulikiwe kwanza ndo tutajua nani ni domo kaya na nani ni mtu mzuri”.

Aidha, alisema katika malalamiko yanayotokea ya uadilifu na uwajibikaji, anaamini kwamba yapo maeneo ambayo hayatakuwa na barabara za lami hadi ‘Yesu atakaporudi’.

“Tunatakiwa kubadilika na kuangalia nani atakayeweza kushughulikia changamoto hizi na matatizo ya nchi yetu na siyo kuweka uso wa kiongozi…tunatakiwa kuwaangalia sana na kuwapima wanaotaka kugombea urais, tuangalie utayari wao na uwezo wao,” alisema na kusisitiza:

 “Tusiweke uso wa mtu kwa kuwa tunapewa sukari wala tusiangalie chama cha Askofu Mokiwa, kwa kuwa kimekuwepo muda mrefu bali tuangalie uwezo wa mtu na chama kitakachosema ukweli na si uongo”.

Alisema kwa mwaka huu kuna mambo makubwa katika nchi, ikiwemo suala la Uchaguzi Mkuu na kupatikana kwa Katiba Mpya, lakini wananchi wasirushe panga kwa kutaka vyama vyao vipite.

“Msikubali kudanganywa, msikiuke upendo na nchi kwa sababu ni dhambi, tuwakwepe sana wanaotudanganya maana hawatuambii ukweli na hawatutakii mema,” alisema.

“Tumekuwa tukidanganywa na wanaotaka kuingia katika nafasi hii (urais) na baadaye tunalalamika, sasa tuangalie nani anayefaa na tusikubali kudanganywa kwa sasa ili tusilalamike baada ya uchaguzi”.

Pia, Askofu Mokiwa aliwataka watanzania kutokubali kurubuniwa na wanaofanya kampeni wakiahidi kwamba wakichaguliwa, watawaletea maji na barabara kwa kuwa hiyo ni haki na wajibu wa serikali kwa wananchi wake.

Askofu Valentino Mukiwa


~HABARI LEO

Related

Siasa 3559767136238440540

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item