jaridahuru

Mitandao

KIMATAIFA: UCHAGUZI WA ZAMBIA KUFANYIKA LEO, JE TANZANIA TUNALOLOTE LA KUJIFUNZA KUTOKA KWAO?


Hatimaye leo wananchi wa Zambia wanapiga kura kuchagua Rais wa nchi hiyo, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Michael Sata Oktoba mwaka jana.
Chama tawala cha Patrioyoc Front kinauhakika wa kushinda katika uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka upinzani.
Waangalizi wa kikanda katika uchaguzi huo, wanasema wameridhishwa na maandalizi ya zoezi zima la upigaji kura.Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kati ya Edgar Lungu anayegombea nafasi hiyo kupitia chama tawala na mpinzani wake HAKAINDE Hichilema kutoka United Party for National Development.
Wagombea wote katika nafasi hiyo ya Urais wakati wakijinadi wameahidi kuimarisha mfumo wa elimu nchini humo, kutengeneza ajira. Huku wapiga kura nao wakitumaini kuwa wanasiasa hao watatimiza ahadi zao.Ikiwa ni miaka 50 toka nchi hiyo ilipojipatia uhuru, Zambia imekuwa imara na imeendelea na msimamo wake wa kufanya uchaguzi tangu kumalizika kwa siasa za chama kimoja nchini humo.
Hata hivyo mshindi katika uchaguzi huo wa leo atatumikia kipindi cha miezi 18 iliyobakia, katika awamu iliyobaki, aliyoiacha marehemu Michael Sata, wakati nchi hiyo ikijiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwakani 2016.
Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 12 kamili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni. Tume ya Uchaguzi nchini Zambia imesema zoezi la uhesabuji kura, linatarajiwa kuanza muda mfupi tu baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika, huku matokeo yakitarajiwa kutangazwa katika kipindi cha saa 48.

Related

Kimataifa 927036311964229380

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item