jaridahuru

Mitandao

SIASA: CCM YAMZIMA JANUARY MAKAMBA, YADAI KAULI YAKE INALETA SIASA YA UBAGUZI, YAMTAKA KUOMBA RADHI

 



KAULI ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ya kuwataka wazee waachane na mbio za urais 2015 kwa madai kuwa ni zamu ya vijana, imeelezwa kuwa ni ya kibaguzi na matusi.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Shinyanga mjini, kupitia kwa Katibu Mwenezi, Charles Shigino, kimesema kuwa kauli hiyo ya Makamba inaleta siasa za ubaguzi ndani ya chama.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Shigino alisema kuwa CCM inapiga vita suala la ubaguzi wa aina yoyote ile kwa binadamu, na kwamba kauli ya Makamba inaweza kuleta hatari kwa mustakabali wa chama.
Kwa mujibu wa Shigino, kauli ya Makamba ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli, ni ya kuwabagua wazee kuwa fikra zao hazifai na kuongeza kwamba ni sawa na kuwatusi, hivyo anapaswa kuwaomba radhi.


“Tunamwomba Makamba atambue kuwa ujana sio kigezo cha kuiongoza jamii ya Kitanzania na hasa katika nafasi nyeti ya urais. Ni bora akajifunza kutoka kwa wazee waliokwishawahi kuiongoza nchi.
“Kama kweli Makamba ana nia ya urais, ni bora akajipa muda wa kujifunza na kupata uzoefu wa kutosha wa nafasi hiyo, kwani Watanzania wanajua bila ubishi kuwa ndani ya CCM hana muda wa zaidi ya mwaka na nusu katika uongozi,” alisema.


Shigino aliongeza kuwa Makamba ni kijana mdogo kisiasa, ambaye anatakiwa kwenda kujifunza kutoka kwa wazee waliopo ndani ya CCM, ambao amekuwa akiwadharau.
Wakati huo huo, Gordon Kalulunga anaripoti kutoka Mbeya, kuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya vijana wa chama hicho (UVCCM), wanatumika vibaya na wagombea na kukisemea chama bila utaratibu.


Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM, Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi, aliyasema hayo katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mbeya juzi, wakati wa Baraza Kuu la UVCCM mkoa, ambalo lilifanyika kwa mujibu wa kanuni za umoja huo kwa ajili ya maandalizi ya kumwapisha Kamanda wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Yona Sonelo na makamanda wa wilaya tisa za mkoa huo.


Akionekana kama anamjibu Katibu wa Hamasa wa UVCCM Taifa, Paul Makonda, ambaye hivi karibuni ametoa tamko kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa hafai kuwania nafasi ya Rais wa Tanzania, Madodi alisema inashangaza vijana kwenda mbio na kutoa matamko ambayo yanapaswa yatolewe na vikao vya chama kwanza.


Alisema kuwa vijana wengi wanatembea na wanaotaka madaraka kutokana na kuwa ndio tegemeo la taifa, kwa sababu wanaweza kukimbia huku na kule.
“Ni kipindi kigumu sana kwenu, wakati wetu kina Guninita waliwahi kufutwa uongozi kutokana na tabia zinazofanana na vijana wa leo. Mnatoa matamko bila hata vikao vya chama kutoa maamuzi,” alisema huku akishangiliwa.


Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Mbeya kutoka Wilaya ya Momba, Hassan Nyalile, aliiambia Tanzania Daima kuwa anaunga mkono kauli ya Madodi akisema ni ya kiungozi, na kuongeza kwamba Makonda anatakiwa kujirekebisha na kurudi kwenye majukumu yake.


“Makonda anatakiwa atafsiri vema kauli ya Madodi na kurejea kwenye misingi ya kanuni ili aweze kufanya vema kazi za jumuiya yake ya watoto, badala ya kila wakati kuinuka na kutoa matamko ambayo yanaashiria yupo na kiongozi mmoja mfukoni kutafuta nafasi ya rais mwaka 2015,” alisema.
Makonda ambaye alikuwepo kwenye baraza hilo, ndiye aliyeanza kueleza kuwa vijana wapo ndani ya mifuko ya wanasiasa wakubwa, ndiyo maana inafikia mahali chama hakiwaamini.


Alisisitiza kuwa kuna baadhi wanaomtuhumu kuwa yeye anatumwa na kundi la watu kutoa matamko, jambo ambalo si la kweli, bali anaongozwa na akili zake mwenyewe na kwamba madhara ya magenge ni kujitafutia riziki binafsi.

Related

Siasa 7878020543899406913

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item