jaridahuru

Mitandao

KITAIFA: N/WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALA ANUSURIKA BAADA YA KUZOMEWA NA WANANCHI UBUNGO, MNYIKA AMUOKOA

 



MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amemnusuru Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala asiendelee kuzomewa na wananchi wakati wa  ziara yake ya ukaguzi wa miundombinu ya maji jimboni humo.

Mapema wanachama wa CCM wakiwa na bendera zao, walionekana kupangwa ili kumzomea Mnyika ambaye hata hivyo hakuwajali, badala yake aliendelea kuhutubia mkutano huku Makala akionekana kufurahishwa na hali hiyo.

Mnyika alieleza jinsi alivyowapigania wakazi wa Kimara Mavurunza na maeneo mbalimbali ya jiji kupata maji pasipo kujali itikadi zao za vyama.

Alisema ziara hiyo ya naibu waziri ni matokeo yake ya kumbana Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, pamoja na watendaji wa Kampuni ya kusambaza maji ya Dawasa kuhakikisha maji yanapatikana kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Alisema kama si kushindwa kwa Serikali ya CCM kuzuia wizi wa maji unaofanywa na watu wanaoyauza, hususan viongozi wa serikali, tatizo hilo lisingekuwa kwa kiasi kinachotisha kama ilivyo sasa.

Alimtaka Naibu Waziri Makala ahakikishe wakazi wa Ubungo na maeneo mengine ya jiji wanapata maji kwa kuwa ni haki yao ya msingi, na kwamba wawabane watu wanaouza maji.
Baada ya Mnyika kumaliza, Makala alisimama na kabla hajaanza kuzungumza wananchi walimueleza kuwa hawataki porojo zaidi ya maji.

“Kiongozi hapa tunataka maji, hizo porojo zako za kisiasa peleka huko huko kwa kuwa tumechoka na ahadi zisizotekelezeka kwa muda wa miaka hamsini,” alisema mwananchi ambaye hakufahamika jina.

Makala badala ya kutulia, alimueleza mwananchi huyo kuwa kama hataki porojo aondoke katika mkutano hali iliyozua zomea zomea kutoka kwa wananchi.
Akiwa amekasirika, Makala aliwatishia wananchi kuwa atawakamata kwa kuwaita polisi, lakini kitisho hicho hakikufua dafu.

Katika jitihada zake za kuendelea kuwatisha wananchi, Makala aliinuka mithili ya kutaka kuwafuata, lakini Mnyika alimzuia na kumueleza hali hiyo isingekuwepo kama CCM wasingeingiza siasa katika masuala ya kiserikali.

Mnyika aliwasihi wananchi wampe nafasi kiongozi huyo aweze kuwaeleza mipango ya serikali.
Baada ya ombi hilo, wananchi walitulia na Makala akaeleza kuwa serikali imeshatenga sh. bilioni 362 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Ruvu Juu na Chini na kwamba miradi hiyo itakamilika ifikapo Septemba mwakani.

Related

ELIMU: JE UMEWAHI KUWA NA NIA YA KUAZISHA SHULE? BASI FAHAMU VIGEZO VYA KUFUNGUA SHULE NA UTARATIBU HAPA

WE NI MJASIRIAMALI, UNATAKA KUFUNGUA SHULE, UTARATIBU MWEPESI NI HUU. Na  Bashir  Yakub. Wapo Watanzania ambao ndoto zao ni kumiliki shule. Ninapoongelea shule simaanishi lazima&nb...

AJIRA: JE UNAKIPAJI CHA UTANGAZAJI? OK..AIRTEL INATAFUTA MTU MWENYE KIPAJI CHA UTANGAZAJI SOMA HAPA UJUE

Je, una kipaji cha kuwa TV Presenter? Tuma video yako katika ukurasa wa Airtel Facebook (www.facebook.com/AirtelTanzania) ukitaja jina lako, unapoishi, umri wako na kitu gani kinachokufanya...

BURUDANI: KWELI MUZIKI UNALIPA!! CHEKI MAFANIKIO YA RECHO WA THT, ADAI YEYE HANA MPANGO NA KUHONGWA

Muimbaji wa muziki kutoka THT, Recho ameweka wazi baadhi ya matunda aliyovuna kupitia muziki wake. Akizungumza jana kwenye kipindi cha Sporah Show, Recho alisema anashukuru Mungu kazi anayofanya t...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item