KIMATAIFA: WANAWAKE 60 WAJINASUA KUTOKA KWA BOKO HARAM, SERIKALI YASHANGAZWA YAITISHA UCHUNGUZI
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/07/kimataifa-wanawake-60-wajinasua-kutoka.html
Maafisa wa usalama wa Nigeria wamesema kuwa zaidi ya wanawake 60
wakiwemo wasichana wa umri mdogo wamekewpa kutoka kwa wanamgambo wa Boko
Haram waliokuwa wamewateka nyara.
Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68 waliotekwa mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa kaskazni mashariki mwa jimbo la Borno.serikali ya Nigeria imeitisha kufanywe uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka wasichana hao.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai
kuwa huenda wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara
walipokwenda kushamblia kambi ya kijeshi. Msemaji wa jeshi la Nigeria
amesema kuwa Ijumaa hiyo (4 Julai) walifanikiwa kuwaua wapiganaji zaidi
ya 50 karibu na mji wa Damboa.