JAMII: NJEMBA YAPOKEA KIPIGO KIKALI KWA KUFUTURU KABLA YA MUDA HUKO DAR ES SALAAM

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/07/jamii-njemba-yapokea-kipigo-kikali-kwa.html

JAMAA mmoja amejikuta katika wakati mgumu baada ya kushushiwa kipigo cha mbwa mwitu alipokutwa anakula kabla ya muda wa futuru hku akiwadanganya wenzake kuwa amefunga.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Jana majira ya saa 8 mchana katika maeneo ya Malapa Jijini Dar es salaam.
Shuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa watu walianza kumvamia jamaa huyo kwa maneno makali ya kuikashifu dini yao na baadae kumshushia kipigo wakidai kuwa ni sawa na kafiri kwa kujifanya amefunga kumbe anakula mchana.
Katika tukio lingine huko Sherifu shamba jijini dar es salaam, Jamaa mmoja ameshushiwa kipigo na wamiliki wa hosteli za Datastar baada ya kukutwa akiwa chumbani katika hosteli ya wasichana ya chuo hicho.
Mtu huyo ambae alionekana kibaka, alipokea kichapo kikali na kisha kutolewa nje na kufikishwa katika kituo cha polisi akidaiwa kuwatishia maisha wanafunzi wanaokaa katika hosteli hiyo.