JAMII: MAKUBWA YA MDADA ALIYEKUTWA KALALA NDANI YA SANDUKU LA KUUZIA CHIPSI YOMBO VITUKA
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/07/jamii-makubwa-ya-mdada-aliyekutwa.html
Asubuhi ya tarehe 08/07/2014, huko yombo vituka kilitokea kutuko cha ajabu baada ya muuza chipsi kuamka asubuhi na mumkuta mdada amelala katika sanduku la kuuzia chipsi. Hata hivyo pamoja na watu kujaribu kumuongelesha, aliondoka kimya bila kujibu.
Jarida Huru imejaribu kulifuatilia tukio hilo kwa undani lakini hatukuweza kuupata ukweli wa tukio hilo kwa kuwa yule dada hakuonekana wa kufahamika alipoelekea.
Hata hivyo muuza chipsi huyo pia hakuwa tayari kutoa ukweli wa jambo hilo. Mashuhuda wa tukio walisema yao na kudai kuwa kitendo hicho huenda kikahusishwa na imani za kishirikina kwani ni cha ajabu. Waliongeza kuwa huenda jamaa huyo akakosa wateja kwa kuwa asilimia kubwa ya wateja wake walipatwa na hofu kwa kudhani kuwa jamaa huyo anatumia nguvu za giza kuwavuta wateja wake.
"Huenda huyu jamaa anatumia sangoma kwenye biashara bwana, inakuwaje mtu tu from nowhere aje aingie kwenye sanduku lako la chipsi, aah! haingii akilini, afu hata mshikaki mmoja asile? hapa kuna kitu" Kilidai chanzo kimoja.
Bado tunaendelea na upekuzi kwani letu sisi ni Jarida Huru hivyo ukweli tutafahamu