BURUDANI: MAMA DIAMOND ASHANGAZWA NA TABIA YA MABINTI KUJITONGOZESHA KWA MWANAE, HAYA NDIO ALIYOSEMA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/07/burudani-mama-diamond-ashangazwa-na.html
MAMA mzazi wa nyota wa muziki wa kizazi kipya,
Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ amesema baadhi ya
wasichana wanajitongozesha kwa mwanaye kwa kuwa ni mtu maarufu.
Mama Diamond amesema wasichana wamekuwa na tabia ya kutumia hata namba yake ya simu na kutuma picha za utupu kwake na kwa mwanaye.
“Napata shida kwa kweli, wasichana wanajitongozesha kwa kupitia namba yangu ya simu, mtu anakupigia anamuulizia Diamond na wengine ndiyo wanatuma hadi picha za utupu kwa kutumia hii mitandao ya kijamii wenyewe wanasema,” alisema.