jaridahuru

Mitandao

WC 2014: NIGERIA YASONGA HATUA YA MTOANO LICHA YA KUFUNGWA 3-2 NA ARGENTINA, MESII ATUPIA 2. CHEKI MAGOLI HAPA

 

SUPASTAA Lionel Messi Leo ameifungia Argentina Bao 2 wakati ikiwafunga Nigeria Bao 3-2 kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi F la Fainali za Kombe la Dunia lakini Nigeria wamesonga Raundi ya Pili ya Mtoano pamoja na Argentina waliokuwa tayari wametinga huko kabla ya Mechi hii.

Ingawa Matokeo haya ni mabaya kwa Nigeria lakini wamesaidiwa sana baada ya Bosnia-Herzegovina, ambayo ilikuwa tayari imeshatolewa nje ya Mashindano haya, kuwatandika Iran Bao 3-1 na kuyakata matumaini ya Iran kufuzu badala ya Nigeria.

Bao za Mechi hii zilifungwa na Messi, Bao 2, na Marcos Rojo kwa Argentina huku Nigeria wakipiga Bao zao zote 2 kupitia Chipukizi wao Ahmed Musa anaechezea Klabu ya CSKA Moscow huko Urusi.

Kwenye Raundi ya Pili ya Mtoano, Argentina itacheza na Mshindi wa Pili toka Kundi E na Nigeria kushindana na Mshindi wa Kundi E.




Related

Worldcup 2014 1355003995225402768

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item