KITAIFA: UKWELI KUHUSU TAARIFA ZA KUFARIKI DUNIA KWA WAZIRI WA ELIMU DR. SHUKURU KAWAMBWA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/kitaifa-ukweli-kuhusu-taarifa-za.html
Ndg Watanzania,WanaBagamoyo na wapenda maendeleo, kwa niaba
ya CCM-Bagamoyo na Ofisi ya Mbunge-Jimbo la Bagamoyo napenda kuleta
kwenu Masikitiko yetu kwa niaba ya Chama na Familia ya Mheshimiwa Mbunge
Shukuru Jumanne Kawambwa kutokana na Usumbufu ambao umesababishwa na
habari zinazoenezwa Mitandaoni (siyo JARIDA HURU) kwamba Mheshimiwa Kawambwa amekumbwa na
Umauti akiwa njiani anaelekea Mwanza. Taarifa hiyo sio ya kweli.
UKWELI
Mheshimiwa Shukuru Jumanne Kawambwa yupo Nchini Canada Akitimiza majukumu yake. Hivyo Watanzania na wana Bagamoyo mnaombwa radhi kwa usumbufu uliotokea na kwamba Mheshimiwa Mbunge yuko na Afya njema na utekelezaji wa Majukumu unaendelea kama kawaida.

Ndg.Ridhiwani Kikwete (Mnec)
Mbunge -Chalinze
Mbunge -Chalinze