jaridahuru

Mitandao

KIMATAIFA: WANNE JELA KWA KUFANYA MAPENZI YA JINSIA MOJA , LICHA YA SHERIA KUTOWEKA WAZI KOSA HILO - MISRI


Mahakama moja nchini Misri imewahukumu watu wanne kifungo cha hadi miaka minane jela kwa kosa la vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja.
Watu hao wanashutumiwa kuhudhuria au kupanga tafrija za vitendo vya ngono, na kuvaa mavazi ya kike na kujipodoa.
Sheria ya Misri haitamki kupiga marufu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, lakini waendesha mashitaka wametumia sheria ya Misri inayokataza mambo fulani kufanyika hadharani kuwahukumu wapenzi wa jinsia moja.

Hukumu hiyo imeshutumiwa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Mmoja wa watu hao amehukumiwa na mahakama mjini Cairo, kifungo cha miaka mitatu jela na kazi ngumu.

Kikundi cha kutetea haki za binadamu chenye makao yake nchini Marekani, Human Rights First , kimesema hukumu hizo zinasikitisha na kukatisha tamaa.

"Misri ni taifa linalobadilika katika eneo la nchi za Kiarabu; kinachotokea Misri kinaweka hali ya kuenea katika ulimwengu wote wa nchi za Kiarabu," kimesema kikundi hicho katika taarifa yake.
Kikundi hicho kimesema tangu kung'olewa madarakani Rais Mohammed Morsi mwezi Julai 2013 kumekuwa na ongezeko la watu kukamatwa kwa misingi ya jinsia zao.

Hukumu ya sasa inakumbushia kesi ya mwaka 2001 ya watu 52 kushutumiwa kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na makosa mengine chini ya sheria ya Misri.

Watu ishirini na watatu walihukumiwa kifungo cha kufikia miaka mitano jela pamoja na kazi ngumu, hukumu ambayo ilishutumiwa kimataifa.

Kikundi kimoja cha kutetea haki za binadamu nchini Misri kimesema adhabu kali zilizotolewa kwa watu hao Jumatatu ni sehemu ya msako unaoendelea dhidi ya uhuru binafsi.

Related

KIMATAIFA: ISRAELI YAANZA MASHAMBULIZI UPYA GAZA BAADA YA KUISHA MASAA SABA YA KUSITISHA MAPIGANO

Majeshi ya Israel imeanza tena upya operesheni yake ya mashambuzi katika eneo la Gaza baada ya kumalizika kwa saa 7 za kusitisha mapigano lililotolewa na na Israel kwa ajili ya huduma za kibi...

KIMATAIFA: RAIS OBAMA ATANGAZA KUPANUA WIGO VIKWAZO DHIDI YA URUSI

  Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kupanua uwigo wa vikwazo dhidi ya Urusi kufuatia mgogoro unaoendelea Ukraines.Tangazo hilo la Rais Obama linafuatia vikwazo vilivyotangazwa na Jumu...

KIMATAIFA: ISRAEL YASEMA ITAJILINDA NA KIKUNDI CHA HAMASS, YASEMA ITALISABARATISHA KUNDI HILO

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inatakiwa kujiandaa kwa ajili ya mpango wa muda mrefu katika Gaza. Hata hivyo ameelezea msimamo wake dhidi ya kundi la wapiganaji wa Hamas...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item