KIMATAIFA: BOKO HARAM WAZIDI KUITEKETEZA NIGERIA, WASHAMBULIA VIJIJI NA MAKANISA MENGINE TENA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/06/kimataifa-boko-haram-wazidi-kuiteketeza.html
Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia vijiji kadha na makanisa kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mashambulio yamefanywa karibu na mji wa Chibok, ambako wasichana wa shule zaidi ya 200 walitekwa nyara mwezi wa Aprili.
Mwandishi wa BBC Nigeria anasema katika kijiji kimoja cha Kautikari, wanamgambo wa kijiji walizidiwa nguvu walipojaribu kulinda kanisa.
Anasema jeshi halikuweza kufika katika vijiji hivyo vilioko mbali.