jaridahuru

Mitandao

ZITTO: Wabunge wanatumiwa na wafanya biashara wakubwa


WAFANYA BIASHARA wakubwa wanadaiwa kuwatumia baadhi ya wabunge kuhakikisha muswada wa kufuta misamaha ya kodi haupelekwi bungeni.

Tuhuma hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu ya Serikali (PAC), Zitto Kabwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuwasilisha taarifa yake.
Zitto alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakishirikiana na wabunge kukwamisha kuletwa kwa muswada huo.

Alisema baadhi ya wabunge hao wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa makampuni ya uchimbaji wa madini kuwakwamisha.
Kwa mujibu wa Zitto, endapo muswada huo utafika bungeni na kuwekwa kuwa sheria wafanyabiashara hao watafutiwa kodi hivyo wamekuwa wakiogopa.

“Ndugu zangu tusaidieni kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wabunge kufanya hili,’’ alisema.

Aidha mwenyekiti huyo alisema pia Songas imekuwa ikidaiwa kwa muda mrefu lakini haitaki kulipa deni lake ambalo limekuwa likizidi kuongezeka.

Alisema Songas wamekuwa wakilalamika kuwa nao wanaidai Shirika la Umeme Tanesco.
“Hawa watu wamekopa fedha serikalini zaidi ya bilioni 238 lakini sasa hawataki kurejesha na hizi ni pesa nyingi ni lazima zirudi serikalini,’’ alisisitiza.

Pia Mwenyekiti huyo alitaka serikali kutumia mashine za kodi, EFDs katika malipo yake jambo ambalo litasaidia kuokoa fedha nyingi.

CHANZO: HABARI LEO

Related

SIASA: MBUNGE WA CCM DODOMA ATANGAZA KUNG'ATUKA, ALITUMIKIA JIMBO KWA MIAKA 20

MBUNGE wa Chilonwa, Hezekiah Chibulunje (CCM), ametangaza kutogombea tena ubunge wa jimbo hilo mwakani baada ya kulitumikia kwa miaka 20 mfululizo. Chibulunje alisema jana kuwa anastaafu u...

KITAIFA: MJANE AFANYIWA UKATILI NA SHEMEJI ZAKE KWA KUINGIZIWA MTI MKAVU SEHEMU ZAKE ZA SIRI WAKIMTAKA AHAME

MJANE mmoja (jina linahifadhiwa kwa sababu za maadili) (24) mkazi wa Kijiji cha Omuga, Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara amefanyiwa ukatili wa kutisha wa kusimikwa kijiti sehemu zake za siri na shemeji...

JAMII: MFANYA BIASHARA WA MADINI MJINI ARUSHA ASABABISHA AJALI MBILI KISHA AJIUA KWA KUJIPIGA RISASI

Mfanyabiashara wa madini, Richard Lucas (29) anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi kichwani baada ya kusababisha ajali mbili tofauti. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema a...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item