jaridahuru

Mitandao

DAR: Ajifungua mtoto na kumtupa chooni, akamatwa na kufikishwa polisi



MWANAMKE MMOJA aliyefahamika kwa jina la Hadija Mohammed, mkazi wa Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam amefikishwa polisi baada ya kufanya kitendo cha kinyama kufuatia kujifungulia kwenye ndoo na kisha kukitupa kichanga  chooni.

Kwa mujibu wa chanzo, mwanamke huyo alionekana kuwa na ujauzito uliotimiza miezi tisa na majirani zake waliuona, lakini siku ya tukioalionekana tofauti kimaumbile jambo ambalo liliwatia wasiwasi ndugu zake na hivyo kulazimika kufanya uchunguzi.


Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa baadhi ya ndugu na majirani walipomuona bila ujauzito walimbana kwa kumuuliza iliko mimba hiyo.“Ndugu zake na majirani walipomuona hana tumbo kama mwanzo walishangaa, wakaamua kumbana tena kwa vitisho kwamba watampeleka polisi.
“Ndipo alipoamua kueleza ukweli kwamba, alijifungulia kwenye ndoo lakini mtoto alikwenda kumtupa chooni,” kilisema chanzo hicho.

Habari zilizidi kudai kuwa baada ya majirani na ndugu kuambiwa hivyo walikwenda kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi Pangani kilichopo Ilala, Dar ambapo walifika na kukiokoa kichanga hicho lakini walikuta kimeshakata roho.

Mpashaji wetu alizidi kudai kuwa, baada ya polisi kuuchukua mwili wa mtoto huyo hawakumwacha mama mtu aendelee kuponda maisha uraiani, walimbeba mpaka kituoni hapo na kumfungulia jalada lenye namba ILA/RB/1715/2014 kisha kumpeleka kwenye Mahabusu ya Polisi Msimbazi huku mwili wa mtoto huyo ukipelekwa Hospitali ya Amana na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Afande mmoja ambaye aliomba jina lake lisiandikwe, alisema ni lazima Hadija apambane na mkono wa sheria ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wenye mchezo huo.

“Hii tabia imekua sana. Wanawake wengi wanajifungua kisha wanawatupa watoto chooni au kokote kusikojulikana ili wao waendelee kula raha mjini. Huyu lazima sheria ishike makali yake ili iwe fundisho,” alisema afande huyo.

CHANZO : JF

Related

Jamii 2939648653279604213

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item