jaridahuru

Mitandao

TISS: Mauaji ya maafisa usalama Tanzania tishio kwa usalama wa raia

Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa
Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa
na watu wasiojulikana katika mazingira ya
kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake
zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika
mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini
Dar es salaam.
Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa
tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na
briefcase ya marehemu huyo ambayo
haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo,
kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili
waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi
kuelekea katika gari yake.
"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru
aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda
kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake
na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema
mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa
Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla
ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.
Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3
la leo Alhamisi, Mei 1 2014.
Siku za karibuni katika tukio lingine  huko mbeya AFISA Usalama wa Taifa mstaafu wa mkoani
Mbeya Joseph Mwasokwa (76) alikutwa amekufa baada ya
kuchinjwa nje ya nyumba yake eneo la Block T ,
Mbeya mjini. Tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia
siku ya Uhuru wa Tanganyika, Disemba 9, 2012,
baada ya mwili wake kugundulika saa 12.45
Asubuhi. Akisimulia mkasa huo, mtoto wa kiume wa
marehemu Mwasokwa, Mpoki Mwasokwa (37),
alisema kuwa Baba yake aliondoka nyumbani siku
ya Jumamosi Desemba 8, mwaka huu kwenda
kuangalia mpira ligi ya Uingereza.

Related

Jamii 6861249903117952750

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item