jaridahuru

Mitandao

TEKNOLOJIA: USIDANGANYIKE NA HII PICHA YA BILLGATES KUKUPA $5000 UNAPO 'SHARE' HII PICHA


Wapendwa, najua hii picha sio mara yako ya kwanza kuiona katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Na kama ndio mara yako ya kwanza, basi unabahati kukutana na ujumbe ujumbe huu sasa.
Hii picha inamuonesha aliyekuwa mtendaji mkuu wa kampuni ya Microsoft na aliyewahi kushika rekodi ya kuwa mtu tajiri zaidi duniani Bill Gates akionesha picha yenye ujumbe kuwa utakapo 'share' hii picha atakupa $5000.

Huu ni uongo na Gates wala hana taarifa kuwa picha yake inatumika katika kuwahadaa watu katika mtandao huo.

Picha hii imefanyiwa marekebisho (Editing) kutoka katika moja ya picha alizo piga katika kongamano la Reddit "Ask Me Anything"  akiwataka watazamaji kuweza kumtambua kwa picha ya kikaragosi ili kumuuliza maswali kuhusu shirika lake la Bill & Melinda Gates Foundation.



Hivyo kuwa makini na nyenzo hizi hatari zinazotumiwa na watu wajanja wanaotaka kujipatia umaarufu kupitia migongo ya watu. Aidha, watu hawa pia wanaweza kukuomba taarifa zako za kibenki, CHONDE CHONDE usiwape taarifa hizo maana ni hatari kwa kuwa wanaweza kukuibia.

Ujanja huu umekuwa unazidi katika mitandao hasa katika email. Pia kuwa makini na watu wanaokutumia meseji facebook wakikuambia uwajibu kupitia email zao. Hayo yote ni ujanja tu wa kutaka kuwa lubuni watu.

Related

Technolojia 7843878657830109761

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item