FA: HATIMAE ARSENAL WAONDOA UTEJA, WATWAA KOMBE LA FA, WADAI NI MWANZO WA ARI MPYA

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/fa-hatimae-arsenal-waondoa-uteja-watwaa.html
Baada ya kukaa muda mrefu bila kutwaa kombe lolote, klabu ya Arsenal imefanikiwa kutwaa ubingwa wa FA baada ya mechi iliyokuwa mshike mshike kwa timu hiyo.
Katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Wembley, timu ya Hull city iliuanzwa mchezo kwa kasi kubwa na kujipatia goli la kwanza katika dakika ya tatu ya mechezo kupitia kwa mchezaji wake James Chester. Dakika tano baadae Curtis Davies aliongezea timu yake ya Hull City bao la pili na kuwafanya mashabiki wa Arsenal kupoteza matumaini ya ubingwa.
Arsenal walipata nguvu baada ya Santi Kazola kuifungia bao la kwanza Arsenal kwa mkwaju wa adhabu katika dakika ya 17 ya mchezo.
Hata hivyo mchezo ulizidi kuwa mgumu kwa vijana hao wa wenger hadi mapumziko walikuwa nyuma kwa 2:1. Kipindi cha pili vijana wa arsene walipata goli la kusawazisha kupitia kwa beki wao Laurent Koscielny katika dakika ya 71 ya mmchezo. Timu hizi ziliingia muda wa ziada ndipo Ramsey alipoyarudisha matumaini ya ubingwa kwa kumalizia kazi nzuri aliyoifanya Geroud na kuiandikia bao la 3 Arsenal katika dakika ya 109.
Hadi mchezo unaisha Arsenal 3:2 Hull.
