BUNGENI: BUNGE LA EAC KURINDIMA KUANZIA KESHO HUKO ARUSHA KUJADILI BAJETI YA 2014/2015
![](https://resources.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
https://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/bungeni-bunge-la-eac-kurindima-kuanzia.html
Arusha. Bunge la Afrika Mashariki (Eala), linaanza vikao vyake kesho. Bunge hilo lilivunjika Aprili Mosi mwaka huu kutokana na vurugu zilizosababishwa na hoja ya kumng’oa Spika Margrethe Zziwa.
Pamoja na mambo mengine, vikao vya Bunge hilo vinavyoanza kwa wabunge kukutana kwenye kamati mbalimbali, litajadili na kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha ya 2014/2015.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Sekretarieti ya EAC, Richard Othieno-Owora alisema jana kuwa Spika Zziwa, ambaye tayari wabunge 37 wametoa hoja ya kutokuwa na imani naye ndiye atakayeongoza vikao.
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC, Phyllis Kandie, ndiye atakayewasilisha Bajeti ya EAC inayotarajiwa kuongezeka kutoka Dola milioni 131.8 bilioni za mwaka jana.
Miongoni mwa miradi na maeneo inayotengewa fedha kwenye bajeti ya EAC ni kilimo, biashara, ulinzi na usalama, miundombinu na elimu.
Wabunge 33 kati ya 45 waliwasilisha hoja ya kumng’oa Spika Zziwa, lakini haikujadiliwa.