jaridahuru

Mitandao

MV NYERERE UPDATE: MARINE ENGINEER ALIVYO NUSURIKA KIFO BAADA YA KUKAA ZAIDI YA MASAA 48 KWENYE MAJI



Majira ya Saa 5:22 Asubuhi Septemba 22,2018 Licha ya kivuko cha Mv Nyerere kuzama majini zaidi ya saa 48 zilizopita wilayani Ukerewe, Alphonce Charahani, mmoja wa Mainjinia wa Kivuko cha Mv.Nyerere kilichopata ajali ya kuzama ziwa Victoriaameokolewa muda mfupi uliopita akiwa hai japo hali yake ni mbaya lakini anapatiwa huduma. 

Injinia huyo ametolewa akiwa hai na kukimbizwa Kituo cha Afya cha Busya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara. Mmoja wa wazamiaji Daniel Kondoyo amesema tangu juzi Septemba 20, 2018 kilipozama kivuko hicho kila walipokuwa wakigonga walisikia mtu mwingine akigonga kwa ndani. 

Baadhi ya wazamiaji wanaoopoa miili wamesema Charahani alikuwa amejipaka oili mwilini ambayo wameielezea kuwa husaidia maji yasiweze kupita katika vinyweleo. Kandoyo amesema kutokana nahali hiyo huenda aliyekuwa akigonga kwa ndani ni Charahani.
 
 Lakini hawezi kuongea kutokana na haliyake kuwa mbaya baada ya kukaa ndani
ya maji kwa takribani siku tatu. Tangu asubuhi leo, miili 30 imeopolewa na kufanya idadi ya miili iliyoopolewa hadi sasa kufikia 166 baada ya mili mingine 136 kuopolewa hadi jana jioni.
 
Miili yote iliyoopolewa imehifadhiwa katika Kituo cha afya cha Bwisya. Miili 116 kati ya 151 iliyoopolewa baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018 imetambuliwa na ndugu. Saa 4:30 Asubuhi Septemba 22,2018 Miili mingine minne imeopolewa na kufanya jumla ya miili 26 kuwa tayari imeopolewa leo. Zoezi linaendelea. 

Baadhi ya ndugu ambao jana walikataa majeneza ya kuzikia jamaa zao waliofariki katika ajali hiyo, wamebadili maamuzi yao na kuanza kudai wapewe majeneza. Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania imetoa mchango wa shilingi milioni 10 kwaajili ya kutengeneza majeneza 100, fedha amekabidhiwa RC Mongella naye kamkabidhi Mhazini. 

Waziri Jenista Mhagama amesema fedha zitaingizwa kwenye akaunti ya maafa itakayotangazwa. Saa 2:34 Asubuhi Septemba 22,2018 Miili mingine mitano imeopolewa na kufikisha jumla ya miili 21 kwa siku ya Leo na kufanya jumla ya miili 157 iliyoopolewa hadi sasa.

Saa 2:20 Asubuhi, Septemba 22 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amesema Miili mingine 16 imeopolewa na kufanya jumla ya watu 152 waliofariki dunia kwenye ajali hiyo huku akibainisha kuwa zoezi la uokoaji linaendelea Aidha amesema kuwa katika zoezi la utambuzi miili 116 imeshatambuliwa na ndugu zao. Katika Hatua Nyingine Mongela amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kutolewa kiasi cha shilingi laki tano kwa kila familia ambayo imepotelewa na ndugu yake.

Na Mwandishi wetu (Ukerewe)

Related

Kitaifa 4452113106806954301

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item