jaridahuru

Mitandao

JH STORY: NILIVYO AMBUKIZWA UKIMWI (DAR)


TABATA
October 06, 2009 Siku ya Jumanne.
Background:
Nilikuwa nimemaliza zangu chuo MUCCoBS kozi ya BAF na kufanikiwa kupata GPA nzuri tu ya 4.2. Nilikuwa na matumaini na ndoto nyingi za mbeleni juu ya maisha yangu. Nilipenda sana elimu na nilitegemea kupata nafasi ya TA (Tutorial Assistant) chuoni hapo. 

Wakati nangojea graduation ambayo huwa mwezi November, nilikuja Dar es salaam kumtembelea dada yangu ambaye alikuwa akiishi huku, Tabata! Naye ndo kwanza alikuwa na mwaka mmoja kazini ila kwa bahati (nzuri?mbaya?...sijui) alipata uja uzito na mshkaji mmoja hivi walisoma naye chuo. 

Basi nikawa nakaa naye pale huku nikingojea siku zisonge.

October 06, 2009 siku ya Jumanne:
Siku hii alitakiwa kwenda clinic na kwa vile alikuwa karibu sana na kujifungua hakuweza kuendesha gari ikabidi nimsindikize kwenye zahanati moja pale Tabata nimeisahau jina.
 
Basi wakati namngojea nikaenda kukaa kwenye mabenchi Fulani pembeni pale kuangalia TV. Karibu yangu alikuwa amekaa binti mmoja mrembo sana kwa kweli. Sikufahamu yupo pale kufanya nini. Nilidhani na yeye kaja kumsindikiza ndugu yake labda. 

 Mimi bila hiyana nikaacha kuangalia TV nikaanza kupiga stori za hapa na pale. Tukakonekt vizuri na kuchangia changia mada iliyokuwa inaonyeshwa kwenye TV. Baada ya kama nusu saa dada naye akatoka ndani akaja tuondoke. Nikamwambia dada kama hutojali unipatie namba yako tuzidi kuwasiliana. 

Baada ya siku ile tuliendelea kuwasiliana sana tu. Tulikuwa tuna chat mpaka ma saa sita ya usiku na ukizingatia sikuwa na kazi. Aliniambia yupo chuo mwaka wa tatu anasoma Sheria.

Moyoni nilihisi hapa nimepata mtu lakini kama nilivyofundishwa sikuwa na papara ya kumtamkia hayo. Bado ninakumbuka maonyo niliyopewa juu ya jiji hili la Daslam!

Baada ya wiki mbili hivi tulikutana for lunch posta..enzi hizo break point bado mpya kabisa. Tuliongea mengi about life.
Tabata:

Wiki moja kabla ya graduation nilimwambia naenda zangu Moshi wiki ijayo hivyo ningependa tuonane. Alikubali na kuja Tabata jioni. Tulikaa tukala na kupiga stori mpaka mida kama saa sita ivi. Nikatumia mbinu za medani za kivita kumshawishi kwamba kwenda hostel kwao mida hiyo ingekuwa ngumu ilhali tungeweza kuchukua tu chumba hapo asubuhi arudi chuoni. Of course, strawberry lips na contessa vilichangia kunisaidia kumfanya akubali. Ila alikuwa amekataa sana mwanzoni.

Tulienda guest moja inaitwa MUNGU ANAKUONA GUEST HOUSE & RESTAURANT. Nikalipa, tukaingia ndani. 

Kazi ikaanza kuomba game ila haikuwa ngumu…long liiive govinder kumar! Basi purukushani za hapa na pale za kujiandaa na game na mimi kwa kuwa nilichanganya Contessa gin na White horse nikasahau kabisaaa matumizi ya kinga.
Nikaenda zangu graduation November na kurudi. Nikawa nimempotezea kabisa Yule binti kama ilivyo kawaida yetu baada ya kupata tunda.
Jana, March 17 2013 Jumapili:
SMS: “Ndugu yangu, kama umenichunia sawa ila mbona hata sikuoni tena hospitali?”
 
Nikashtuka hospitali? Si ikabidi nimpigie!!!
Ananiambia: “Si pale Tabata sikuoni ukija tena kuchukua ARVs”
Conclusion:
Kumbe benchi nililokuwa nimeenda kukalia ile siku lilikuwa la wagonjwa wa UKIMWI na yeye alikuwa akisubiri kuchukua dawa.
Mimi nikamwambia acha kunidanganya mbona wewe unaishi hostel Kigamboni na ninajua hivyo..yani huko kote hakuna dispensary?
Akaniambia wagonjwa wengi hawaendi kuchukulia dawa karibu na kwao kwa kuhofia kunyanyapaliwa hivyo alijua na mimi nipo kwenye foleni ya kuchukua dawa ndiyo maana hakuona umuhimu wa kunilazimisha kutumia kinga.
Nilishtuka...nikazimia…ndo nimeamka leo...
Wasalaam wapendwa,
Mentor.
 
WRITER: MENTOR

Related

JH Story 2159945609894022547

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item