jaridahuru

Mitandao

MIKATABA YA LESENI ZA UDEREVA TANZANIA: UHABA WA "MATERIAL" AU CHANGA LA MACHO?


Baada ya sekeseke la hivi majuzi kuwa madereva wa Tanzania wanapaswa kutembea na vyeti vyao vya shule ya udereva kwenye magari na kuibui hisia za watu wengi kuhusu uhalali wa kisheria wa hatua hiyo, madereva wengi wamehoji upatikanaji wa leseni zao baada ya kuomba.

"Ni takribani mwaka mmoja sasa tangu niombe leseni yangu ya udereva na kupatiwa risiti ya kusubiria leseni ila hazijatoka, kila siku nikienda TRA wanasema bado material hazijaja,. sasa hii karatasi imechakaa na huenda nikaipoteza nashangaa kwanini haziji" Alizungumza mmoja wa madereva alipohojiwa na mwandishi wetu.

Katika Gazeti la The Citizen la November 4, 2017, Lili mnukuu Mkurugenzi wa Mlipa Kodi na Elimu, Ndg Richard kayombo akikiri kuwepo kwa uhaba wa material za kuchapisha leseni na kuahidi kuwa zingeanza kuchapishwa baada ya wiki mbili jambo ambalo hadi sasa ni kizungumkuti.

Ni hakika kuwa sheria ya barabarani inamtaka mtumiaji wa chombo cha moto kuwa na leseni hali na sio risiti ya malipo anapokuwa anatumia chombo cha moto barabarani ili kuthibitisha kuwa ni dereva aliyethibitishwa kutumia chombo hicho.

Muda mrefu umepita sasa tangu tatizo la upatikanaji wa leseni na uhaba wa leseni kuwepo Tanzania, je ni mikataba iliyofichwa? au TRA imeshindwa kumlipa mkandarasi wa kuchapisha leseni hizo?

Kampuni ya SuperCom ndiyo inayo shughulika na kuchapisha leseni hiyo kwa mifumo yao, mkataba ambao hata hivyo haujulikani ni lini uliingiwa au zabuni ipi iliyotolewa kwa kazi hiyo na thamani yake.

Hata hivyo juhudi za JH kutaka kufahamu undani wa taarifa hizi umegonga mwamba baada ya kila aliyeulizwa kuhusu suala hilo kutoa jibu jepesi "karibuni tutaanza kutoa leseni"

Na Mwandishi wetu

Related

Kitaifa 3634846554334047647

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item