jaridahuru

Mitandao

BIASHARA: WAFANYA BIASHARA NCHINI WALIA NA MSAMAHA WA KODI

Picha

MWITIKIO wa wafanyabiashara na walipa kodi wanaojitokeza kuomba msamaha wa riba na adhabu kwenye Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) umeelezwa kuwa ni mkubwa.

Hatua hiyo inafuatia TRA kutangaza mwezi uliopita msamaha wa riba na adhabu kwa wafanyabiashara na walipa kodi wote nchini.

Msamaha huo unatokana na mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya mwaka 2015 yaliyofanywa na Bunge kuingiza kipengele kinachompa mamlaka Kamishna Mkuu TRA kusamehe riba na adhabu hizo za kodi.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo, Richard Kayombo alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa wafanyabiashara na walipakodi wanajitokeza kwa wingi kwenye Ofisi za TRA wakiwa na nyaraka muhimu zitakazowawezesha kupata msamaha huo baada ya kuwasilisha maombi.

Kayombo aliendelea kutoa mwito kwa wafanyabiashara na walipakodi kuomba msamaha huo kuzingatia muda uliowekwa wa kikomo. Agosti 14 mwaka huu, TRA ilikutana na wafanyabiashara na walipakodi Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa elimu ya kodi kwa umma wa wafanyabiashara na walipakodi nchini.

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere aliyewakilishwa na Kaimu Kamishna wa Idara ya walipa kodi wakubwa TRA, Alfred Mregi, alisema msamaha huo wa riba na adhabu unahusu malimbikizo ya kodi.

Ili kuhakikisha hilo linafanyika kwa mafanikio, TRA imetoa miezi sita kuanzia Julai mosi hadi Desemba 31 mwaka huu, kwa wafanyabiashara na walipakodi kupeleka maombi yao ya kusamehewa kodi hizo na adhabu.

Related

Kitaifa 4093906428095199389

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item