jaridahuru

Mitandao

SERIKALI KUTIA MAGUU TEKNOLOJIA MPYA KWA WAKANDARASI WA NDANI

Picha

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema imeandaa utaratibu kusaidia wahandisi wazawa kupata fursa ya kurithi teknolojia kutoka kwa wageni katika miradi mikubwa nchini.

Akizungumza Dar es Salaam juzi wakati akifunga Kongamano la Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Wahandisi sambamba na Siku ya Wahandisi nchini lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa alisema kuwa hivi karibuni Bunge limepitisha sheria ya kumtambua mkandarasi mzalendo na shughuli zake za kihandisi.

“Wizara imekuwa na utaratibu wa kuangalia namna ya kuwasaidia wahandisi wazalendo. Mfano miradi inayofikia Sh bilioni 20 lazima iachwe kwa wazawa peke yake lakini miradi mikubwa tunapoingia mkataba unatengenezwa kwa malipo yanayoweza kuwa kwa fedha za kigeni na malipo ya fedha za Kitanzania ambapo inatoa fursa wageni kuwashirikisha wahandisi wa Kitanzania katika kazi,” alisema.

Alisema, katika ajira, ERB nayo inasimamia eneo hilo kuhakikisha wahandisi wazawa wanahusishwa katika miradi iliyopo nchini, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi sambamba na wageni katika miradi wanayopata hapa nchini, lengo likiwa ni kujenga uwezo na uzoefu mkubwa kwa wahandisi wazawa.

Hata hivyo, Naibu Waziri Kwandikwa aliwataka wahandisi kuzingatia maadili na taratibu za kazi na kuonya wasiofanya hivyo watachukuliwa hatua mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa leseni za uhandisi ili kuepuka maafa yanayoweza kusababishwa kutokana na uzembe katika kazi za kihandisi.

Related

Technolojia 1873587970417155860

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item