BURUDANI: JE UNAMFAHAMU VIZURI YULE VIDEO QUEEN WA NTAMPATA WAPI YA DIAMOND? HUYU HAPA..WANADAI ANAMVUTO ZAIDI YA PENNY!!

https://jaridahuru.blogspot.com/2015/02/burudani-je-unamfahamu-vizuri-yule.html
“Haya sasa, najua mlikuwa mkisubiria kwa mda mreeeeefu, hii ndio Instagram Aacount ya yule dada alonisaliti kwenye video ya #Ntampata_Wapi. .Basi nnavyowajua atatongozwa leo hadi akome, makuwadi sasa,” ameandika Diamond kwenye picha aliyoweka Instagram akiwa na msichana huyo.
Kwenye mahojiano mwezi disemba 2014, Diamond alisema alifurahishwa na jinsi msichana huyo alivyoigiza kwenye video yake.
“Kiukweli amejitahidi na amefanya vizuri sana. Bado tunawasiliana, hata juzi nilimtumia meseji nikamwambia ‘Melissa natamani ujue jinsi gani unazungumziwa, nikasema ‘najua kabisa huko South Africa hawawezi kuwa wanaizungumzia hii video kama wanavyoizungumzia hii video huku nyumbani, natamani ujue jinsi gani walivyokupokea, natamani ujue umefahamika kiasi gani. Nikamwambia ‘siku ntakutag Instagram, halafu utaona shughuli yake.’ Ntamuweka siku moja Instagram, najua watu wanasubiri akaunti yake,” alisema.
Msichana huyo anaitwa Melissa Magiera, na yupo chini ya kampuni ya Ice Model Management, tawi la Cape Town na ‘Ntampata Wapi’ ndio video yake ya muziki ya kwanza kuwahi kufanya.
Kupitia kupitia akaunti yake ya Facebook, October 15 alipost picha ya behind the scenes ya video hiyo na kuandika: 19 hour shoot! Featured in my first music video. Unfortunately I cannot show any other pictures.”
Tazama zaidi picha zake.