jaridahuru

Mitandao

VYUONI: MWANAFUNZI WA SAUT MWANZA APIGWA NA WENZAKE HADI KIFO KWA KUHISIWA KUWA MWIZI


Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) cha jijini hapa, Helma Michael (22)  ameuawa kwa kupigwa mawe na wanafunzi wenzake, wakimhisi kuwa ni mwizi wa kompyuta ndogo za mkononi na deki chuoni hapo. 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Valentino Mlowola, alisema jana kuwa mwanafunzi huyo aliuawa Mei 13 mwaka huu saa 4.00 usiku, katika eneo la Nyamalango Malimbe, ambapo baada ya kubainika katika eneo hilo alianza kupigwa kwa mawe, fimbo na mapanga hadi kusababisha kifo chake.
“Huyu ameuawa katika tuhuma ambazo mpaka sasa hazijathibitishwa,” alisema.  
Kutokana na mauaji hayo, watu 17 wamekamatwa na Polisi  imeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo huku Kamanda Mlowola akiwataka watu kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwaua watu ambao hawana hatia.
Katika tukio jingine, Kamanda Mlowola alisema mkazi wa Kijiji cha Bugula Kata ya Bwiro wilayani Ukerewe, Bazil Amran aliuawa kwa kupigwa na kipande cha ubao kichwani na Parapara Paulo (36)  kwa tuhuma za wizi. 
Kwa mujibu wa Kamanda Mlowola, mauaji hayo yalitokea Mei 12 mwaka huu saa 11 alfajiri  kijijini hapo ambapo alisema mtuhumiwa amekamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.
Aidha katika tukio jingine, Kamanda Mlowola alisema Mei 13 mwaka huu majira ya saa saba mchana katika eneo la Mkuyuni kata ya Mahina wilayani Nyamagana, askari polisi waliokuwa doria waliwakamata Sylvesta Musa (31) na Noela Joseph (34) wote wakiwa ni wakazi wa Mkuyuni wakiwa na bastola aina ya LOCK NO. TZ CAR 91968 ikiwa na risasi tano kwenye magazinie yake.
  

Related

VYUONI: MBUNGE WA CHALINZE, RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI SEKONDARI VITANDA 267

MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekabidhi vitanda 267 katika shule za sekondari za bweni saba jimboni humo vyenye thamani ya sh milioni 53.4.  Akizungumza wakati wa kukabidhi v...

TANZIA: MHADHIRI MKUU MWANDAMIZI WA CHUO CHA SAUT-MWZ, NKWAMBI NG'WANAKILALA AFARIKI DUNIA

Mwanza. Mhadhiri Mwandamizi Idara ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Tanzania (Saut), Nkwabi Ng’wanakilala, amefariki dunia katika Hospitali ya Ru...

VYUONI: ILE KOMEDI YA ELIMU TANZANIA YAFIKIA PATAMU, SERIKALI YAPANDISHA ADA VYUO VYA UALIMU KARIBU MARA MBILI

  Serikali imepandisha maradufu ada kwa wanafunzi wanaosomea ualimu kwenye vyuo vya ualimu nchini kuanzia muhula ujao wa masomo.   Ada hizo kwa wale wa ngazi z...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item