jaridahuru

Mitandao

MICHEZO : TBC1, TBC2 Kurusha kombe la dunia 2014



SHIRIKA la Utangazaji la Taifa (TBC), linatarajia kurusha moja kwa moja ‘live’ mashindano ya Kombe la Dunia kwa mechi zote 64 zitakazochezwa nchini Brazil.
Michuano hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 12, katika viwanja mbalimbali nchini humo na kufikia tamati Julai 13.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu TBC, Clement Mshana, alisema wamefanikiwa kununua haki ya kurusha moja kwa moja mashindano hayo kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Mshana alisema watarusha mechi zote katika runinga za shirika hilo ambazo ni TBC1 na TBC2, pamoja na kituo chao cha redio TBC FM.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha Watanzania wanapata burudani kupitia ving’amuzi mbalimbali ikiwemo Star Times, kwani wana imani kupitia TBC watajua kinachoendelea nchini Brazil.

Related

Michezo 1042142400084811743

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item