jaridahuru

Mitandao

KIMATAIFA: MLIPUKO WAUA 6 NA KUJERUHI WENGINE HUKO KANO NIGERIA


Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 6 na kuwajeruhi wengine wengi.

Shambulio hilo limefanywa katika eneo linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC mjini Abuja Will Ross anasema kuwa eneo hilo lililolengwa linajulikana kama Sabon Gari. Watu wengi walikuwa kwenye migahawa ya vileo na kwenye barabara. Amesema kuwa kilichosalia kwenye gari lililokuwa na bomu hiyo ni injini pekee.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja mji wa Kano umepumzika kutokana na mashambulio, hasa kwasababu ya oparesheni kali iliyofanywa na maafisa wa usalama kuwasaka wanamgambo hao wa Boko Haram.
'Mashambulio ya awali'
Rais Goodluck Jonathan alilazimika kufutilia mbali ziara yake mjini Chibok wiki jana kutokana na utovu wa usalama

Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.

Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.

Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.

Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.

Related

KIMATAIFA: MUGABE HOI TENA, ARUDI SINGAPORE

Rais wa Zimbabwe amarejea tena nchini singapore ili kuangalia afya yake kwa mara nyingine. Hii ni miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa jicho huko huko singapore, hii imedhibitishwa na msemaj...

KIMATAIFA: WATU 157 WAFA KATIKA MGODI WA MAKAA YA MAWE UTURUKI

Mlipuko katika mgodi wa makaa ya mawe magharibi mwa Uturuki umesababisha vifo vya zaidi ya wachimbaji migodi 150 na kujeruhi wengine zaidi ya 70 kwa mujibu wa maafisa nchini humo. ...

KIMATAIFA: SUDANI KUSINI WAKIUKA SAINI YA MAKUBALIANO YA AMANI WAINGIA VITANI TENA

Saa chache tu baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa usitishaji mapigano nchini Sudan kusini Malumbano yameibuka . Sasa Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini wanalaumiana k...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za JuuMitandaoPiga Kura

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item