KIMATAIFA: KIONGOZI WA KUNDI LA MUNGIKI KENYA 'MAINA NJENGA' AMESHAMBULIWA KWA RISASI

https://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/kimataifa-kiongozi-wa-kundi-la-mungiki.html
NYAHURURU, Kenya. Aliyekuwa Kiongozi wa kundi la Mungiki lilowauwa na kuwachinja wananchi wa Kenya katika vurugu za baada ya uchaguzi Kenya, Maina Njenga, ameshambuliwa kwa risasi huko Kenya.
Njenga aliyekuwa katika msafara wa magari mawili alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana wakiwa katika gari dogo. Watu hao waliyashambulia magari yaliyokuwa katika msafara huo na hadi sasa imefahamika kuwa watu watano (5) waliokuwa katika gari moja na Njenga wamefariki.
Njenga amekimbizwa katika Hospitali ya Agha-Khan ya Nyahururu na wawili waliokuwa katika gari lingine wameumizwa vibaya na wamepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Nyahururu.