jaridahuru

Mitandao

"UKAWA HAWAWEZI KUKAA ZIZI MOJA" Nape Nnauye

Dar es Salaam. Siku moja baada ya vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutangaza kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais na ubunge majimboni, CCM kimebeza hatua hiyo kikisema viongozi hao hawawezi kukaa zizi moja.
Akizungumza jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema viongozi wa Ukawa ni genge la wasaka madaraka hivyo hawawezi kuungana kwa hilo.
Nnauye alisema viongozi wa vyama vya upinzani waliungana kwa lengo la kutafuta Katiba bora, lakini wamebadilisha ajenda na sasa wanazungumzia urais mwaka 2015.
“Hawa kumbe ni waongo, malengo yao siyo Katiba, bali ni kutafuta madaraka, muungano wa kutafuta madaraka hauwezi kufanikiwa kwa sababu viongozi wote wa Ukawa ni wapenda madaraka,” alisema Nnauye.
Alisema wananchi watashuhudia umoja huo ukisambaratika kwa sababu viongozi wa Ukawa hawawezi kuvumiliana na kuachiana madaraka.
“Kuungana ni jambo zuri, lakini sababu za kuungana zinapotajwa kuwa ni kumsimamisha mgombea mmoja wa urais mwaka 2015, watasambaratika kabla ya muda huo kufika,” alisema.
Alisema Ukawa wamewadanganya wananchi kwamba wanasimamia Katiba bora kumbe ajenda kuu ni kuongoza nchi.
Gazeti hili jana liliripoti kuwa Ukawa pia wanataka kusimamisha mgombea mmoja wa ubunge katika kila jimbo la uchaguzi.
Katika habari hiyo, Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia walikiri kuwapo mpango huo.
Taarifa za kuwapo mpango, zimekuja siku chache tangu kufichuliwa kwa mpango mwingine wa kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri Kivuli ambalo litawajumuisha wabunge wa vyama vya upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa bajeti unaoanza Mei 6, mwaka huu.

Related

sport 750068575930143467

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item