TEKNOLOJIA: JIFUNZE JINSI YA KUTENGENEZA WINDOWS BOOTABLE FLASH (KISWAHILI & PICHA)
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/teknolojia-jifunze-jinsi-ya-kutengeneza_13.html
Nimekutana na hili swali kwa muda mrefu sasa na ili kuonesha mapenzi yangu ya dhati kwa mafans wangu, leo nakuja na jinsi ya kutengeneza Bootable flash kwa ajili ya kupiga window kwa lugha ya kiswahili.
Hatua hizi ni rahisi sana lakini tafadhali zifuate hatua baada ya hatua kama zilivyo elekezwa na ninakuambia hautopata shida yoyote katika zoezi hili. Iwapo utapata shida katika hatua hizi usisite kuuliza.
VITU UKAVYO HITAJI:
- Flash yenye angalau 4GB
- Computer yenye Windows
- File la Windows 7/8 OS
- Chomeka Flash yako katika computer yako.
- Anzisha programu ya DOS kwa kuandika "CMD" katika eneo la search iwapo unatumia windows 8 au Start iwapo unatumia windows 7.
- Baada ya kuipata programu ya DOS, andika neno "diskpart" katika programu hiyo kisha bonyeza --> Enter
- Utapata kijiprogram cha kuchagua iwapo unahitaji kuianzisha programu hiyo ya diskpart. Chagua 'YES'.
- Ikifunguka subiria kama sekunde kumi kisha andika neno "list disk" kisha bonyeza --> Enter utapata orodha ya disks zilizopo kwenye komputer yako.
- Chagua ile ya flash yako (utaitambua kwa kuangalia capacity yake, yaani ina gb ngapi.) kwa kuandika neno "select disk (andika namba ya flash yako hapa kama ilivyo andikwa katika orodha hapo juu) Mfano: "select disk 1" Kisha bonyeza --> Enter
- Andika neno "clean" ili kuisafisha clusters zake kisha bonyeza tena --> Enter
- Andika neno "create partition primary" kisha bonyeza --> Enter
- Andika neno "select partition 1" kisha bonyeza --> Enter
- Andika neno "active" kisha Bonyeza --> Enter
- Andika neno "format fs=ntfs quick" kisha bonyeza --> Enter
- Andika neno "exit" ili kuondoka katika programu hiyo.
- Baada ya hapo Copy mafile ya ile windows yako kwenye hiyo flash na hadi hapo utakuwa tayari umeshatengeneza Bootable flash tayari kwa kupiga window.