KIMATAIFA: WATU 10 WAPOTEZA MAISHA NA ZAIDI YA 80 KUJERUHIWA KATIKA MILIPUKO YA MABOMU NAIROBI
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/kimataifa-watu-10-wapoteza-maisha-na.html
Matukio ya Kigaidi yameendelea kuigubika nchi ya Kenya ikiwa ni pamoja na milipuko ya mabomu katika sehemu mbali mbali za nchi hiyo.
Leo katika hali isiyo ya kawaida milipuko miwili imeripotiwa
katika sehemu mbili za maeneo ya soko la Gikomba lililoko katika mtaa wa
Eastleigh Huko Mjini Nairobi. Watu 10 wamepoteza maisha na wengine 80 kulazwa
katika hospitali mbali mbali za jiji hilo.
Kamanda wa polisi wa eneo hilo amethibitisha kutokea kwa
milipuko hiyo na kuwaomba watu kuwa watulivu na kumripoti mtu yeyote
wanaemhisi. Hata hivyo hakuna aliyekamatwa kwa kuhusika na tukio hilo ingawa
taarifa za awali zinakihusisha kikundi cha Al-Shabab na tukio hilo.
Mlipuko
wa kwanza ulitokea katika gari la abiria wakati la pili likitokea upande wa
pili wa soko.
Milipuko
ya leo imetokea siku moja baada ya Uingereza kutoa onyo kwa raia wake wanaoishi
nchini humo kurejea makwao kwa hofu ya usalama na pia baada ya tahadhari
kutolewa ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
Gikombaa
ni soko kubwa la kuuza nguo ambalo linapakana na mtaa wa Eastleigh ambako
wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Soko hilo
linapakana na mtaa wa Easleigh ambako wasomali wengi wanaishi na kufanya kazi.
Shirika
la serikali la kushughulikia majanga linasema kuwa angalau watu 10 wamefariki
na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa.