KIMATAIFA: MKE wa Rais Obama akasirishwa na utekaji wa wasichana Nigeria
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/kimataifa-mke-wa-rais-obama-akasirishwa.html
Mke wa Rais wa Marekani Barack Obama Bi. Michelle Obama amesikitishwa na utekaji wa wasichana wa shule uliofanyika April 10 huko Nigeria.
Akiongea kwa niamba ya Rais Obama katika Hotuba ya Rais ya kila wiki, alisema yeye pamoja na mme wake Rais Barack Obama walichukizwa sana na kitendo hicho, aliongeza kuwa kitendo hicho ni cha kinyama na chenye nia ya kuwarudisha nyuma wanawake wanao itafuta Elimu.
Utakaji huo Kundi la Bokko Haram wamethibitisha kuhusika.
Aliendelea kusema kuwa kitendo hicho ni moja ya mikakati ya kudidimiza na kukikandamiza kizazi cha elimu ya kike, akimtolea mfano binti wa Pakistan 'Malala Yousafzai' aliyepigwa risasi na kujeruhiwa akitetea elimu ya mtoto wa kike.
Alisema Ujasiri ulioko ndani ya wasichana kama Malala usipuziwe badala yake upewe kipau mbele kwani ndio ukombozi wa mtoto wa kike.
Pia mapema wiki hii alionekana katika picha yake ya twiiter akiwa ameshikilia bango lililoandikwa "#BringBackOurGirls". Yaani walete watoto wetu nyumbani.
Chanzo : BBC