jaridahuru

Mitandao

TANZIA: WIZARA YA KILIMO YAPOTEZA WATUMISHI 5 KWENYE AJALI YA BARABARANI MANYONI

Watu watano wanadaiwa kupoteza maisha katika ajali ya Gari ndogo, ya Wizara ya Kilimo na Chakula, iliyokuwa imebeba wataalamu wanne pamoja na dereva wote wamefariki papo hapo katika eneo la Njirii Manyoni mkoani Singida leo Jumapili Oktoba 21,2018
.

  Inaelezwa kuwa wanaume ni watatu na wanawake wawili. 

TANZIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anapenda kuwataarifu ya kuwa Wizara ya Kilimo imepatwa na msiba wa Watumishi wake Watano (5) waliopata ajali leo asubuhi tarehe 21 Oktoba, 2018 Manyoni mkoani Singida, walipokuwa safarini kuelekea Mwanza kikazi.

 Watumishi hao waliofariki ni;
1. Stella Joram Ossano (39)
2. Esta Tadayo Mutatembwa (36)
3. Abdallah Selemani Mushumbusi (53)
4. Charles Josephat Somi
5. Erasto Mhina (43)
Miili ya marehemu ipo njiani kuja Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo tarehe 21 Oktoba 2018.

Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi, Amina🙏🏿

Related

Kitaifa 4214947856638893083

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item