WAVUVI WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI MGOGORO BAINA YAO NA WAAJIRI WAO!!
http://jaridahuru.blogspot.com/2016/06/wavuvi-waiomba-serikali-kuingilia-kati.html
ZAIDI ya Wavuvi 1,000 wa Kisiwa cha Kasarazi wilaya ya Sengerema
mkoani Mwanza wameiomba serikali kuingilia kati mgogoro baina yao na
waajiri wao kutokana na kile kinachodaiwa kutoridhishwa na utaratibu wa
malipo yao na kutozwa shilingi laki tatu kwaajili ya uwanja na mashine
kila wanapoingia ziwani.
Ni kisiwa cha Kasarazi kilichopo katika ziwa Victoria wilayani
Sengerema, Kaskazini Magharibi mwa mkoa wa Mwanza, Kisiwa ambacho
kimejizolea umaarufu kwa shughuli za uvuvi wa samaki pamoja na dagaa,
shughuli hizi za uvuvi zimechangia upatikanaji wa ajira kwa asilimia
kubwa ya wakazi waishio pembezoni mwa ziwa Victoria, shughuli ambazo
mara nyingi hufanyika nyakati za usiku.
Licha ya uvuvi kuonekana kuwa mkombozi kwa baadhi ya watu kujipatia
riziki zao za kila siku lakini bado zipo changamoto zinazowakaibili
wavuvi hawa kwa takribani miaka 10, wavuvi wanaona ipo haja ya serikali
kuingilia kati mgogoro baina yao na waajiri wao.
Msilikale Juma ni Katibu wa wamiliki wa Vyombo vya Uvuvi katika
Kisiwa cha Kasarazi yeye anawatupia lawama baadhi ya wavuvi kutokua
waaminifu katika biashara hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akiwa katika ziara yake wilayani
Sengerema anakutana na uongozi huo wa wavuvi pamoja na waajiri wao na
hapa anatoa maelekezo juu ya mgogoro huo.
Kisiwa hicho cha kasarazi wilayani Sengerema kina jumla ya wavuvi
1,165 na waajiri wao 50 ampabo hivi karibuni wavuvi hao Kisiwa hicho cha
Kasarazi Wilayani Sengerema walistisha kufanya shughuli zao za uvuvi
kwa siku nne mfululizo kutokana na mgogoro baina yao na waajiri wao.