GGM KUKABILIANA NA UHABA WA AJIRA!
http://jaridahuru.blogspot.com/2016/06/ggm-kukabiliana-na-uhaba-wa-ajira.html
KUTOKANA na uhaba wa ajira kwa vijana Mkoani Geita, Mgodi wa dhahabu
wa Geita GGM umebuni miradi mbalimbali yenye lengo la kukabiliana na
wimbi hilo ili kubadili na kukuza uchumi wao na jamii kwa ujumla ambapo
zaidi ya vijana 400 wakiwemo wanawake watanufaika.
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ushonaji wa nguo, uchomeleaji ,
kilimo cha kisasa cha mpunga na uzarishaji wa tofari za kisasa, ambapo
Mgodi huo kupitia kwa Makamu wa rais ambaye anashughulika na masuala ya
jamii na maendeleo endelevu ilipo migodi ya Anglogold Ashanti duniani
David Noko amesema mgodi utaendelea kuwahamasisha kuzalisha bidhaa iliyo
bora itakayokidhi masoko yaliyopo nje ya Mkoa wa Geita.
Wakizungumza na CLOUDS baadhi ya vijana waliochukua fursa ya kujiunga
na ujasiliamali katika moja ya mradi uliofadhiliwa na mgodi wa
kuzalisha tofari za kisasa, pamoja na changamoto zilizopo kwa hivi sasa
wamesema wamepokea mradi huo kwa matumaini ya kuwainua kiuchumi.
Awali akizungumza na baadhi ya vijana wakati alipotembelea kalakana
la miradi hiyo, David Noko amesema kwamba miaka kadhaa iliyopita mgodi
haukuwa na ukaribu na wananchi, lakini kwa hivi sasa anafarijika kuona
mabadiliko ya kimahusiano yanaendelea kuonekana.
Pia Kiongozi huyo ametembelea maduka makubwa yanayoshirikiana na
mgodi katika ununuzi wa bidhaa zake huku akidhuru kwenye mashimo
yanayotoa dhahabu ndani ya mgodi wa GGM.