jaridahuru

Mitandao

ZITTO: Wabunge wanatumiwa na wafanya biashara wakubwa


WAFANYA BIASHARA wakubwa wanadaiwa kuwatumia baadhi ya wabunge kuhakikisha muswada wa kufuta misamaha ya kodi haupelekwi bungeni.

Tuhuma hizo zilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu ya Serikali (PAC), Zitto Kabwe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuwasilisha taarifa yake.
Zitto alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakishirikiana na wabunge kukwamisha kuletwa kwa muswada huo.

Alisema baadhi ya wabunge hao wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa makampuni ya uchimbaji wa madini kuwakwamisha.
Kwa mujibu wa Zitto, endapo muswada huo utafika bungeni na kuwekwa kuwa sheria wafanyabiashara hao watafutiwa kodi hivyo wamekuwa wakiogopa.

“Ndugu zangu tusaidieni kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wabunge kufanya hili,’’ alisema.

Aidha mwenyekiti huyo alisema pia Songas imekuwa ikidaiwa kwa muda mrefu lakini haitaki kulipa deni lake ambalo limekuwa likizidi kuongezeka.

Alisema Songas wamekuwa wakilalamika kuwa nao wanaidai Shirika la Umeme Tanesco.
“Hawa watu wamekopa fedha serikalini zaidi ya bilioni 238 lakini sasa hawataki kurejesha na hizi ni pesa nyingi ni lazima zirudi serikalini,’’ alisisitiza.

Pia Mwenyekiti huyo alitaka serikali kutumia mashine za kodi, EFDs katika malipo yake jambo ambalo litasaidia kuokoa fedha nyingi.

CHANZO: HABARI LEO

Related

Habari Mpya 5695145821076772987

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item