SIASA: Kifahamu vyema chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT)
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/siasa-kifahamu-vyema-chama-cha-alliance.html
1.
Utangulizi.
Ndugu
wana habari,
Naomba
nichukue fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito wa kuhudhuria mkutano wetu,
ambao ni wa kwanza tangu chama chetu kianzishwe. Tunatambua na kuheshimu kazi
yenu kama mhimili wa nne wa dola, na leo tunaomba kuzungumza na watanzania
kupitia kwenu.
Lengo
kuu la mkutano huu ni kukitambulisha kwenu chama kipya cha siasa kinachoitwa
Alliance for Change Tanzania (ACT Tanzania) na kuwaombeni kukitambulisha chama
hiki kwa watanzania kupitia vyombo vyenu vya habari.
2.
ACT Tanzania ni nini?
Ndugu
Wanahabari,
ACT
Tanzania ni kifupi cha maneno: Alliance for Change and Transparency,
yaaani Umoja wa Mabadiliko na Uwazi. Ni chama kipya cha siasa kilichoanzishwa
kwa lengo mahsusi la kuwaleta pamoja watanzania wanaoamini kwamba nguvu ya
pamoja inahitajika katika kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi hii, na kwamba
uwazi na uadilifu ni tunu ambazo taifa hili linazihitaji sana kwa sasa na
baadaye.
3.
Itikadi na Misingi ya ACT Tanzania.
ACT
Tanzania ni chama kinachoaamini katika demokrasia jamii na chenye shabaha kuu
ya kupigania na kusimamia mabadiliko na uwazi nchini Tanzania.
ACT-Tanzania
inaamini kuwa mabadiliko yoyote katika jamii lazima yainufaishe jamii husika,
na kwamba wananchi wenyewe ni lazima washiriki katika kuleta mabadiliko hayo
kwa uwazi na uzalendo.
Mwongozo
wa sera za ACT-Tanzania ni maendeleo shirikishi na kuhakikisha uwepo wa uongozi
adili katika ngazi zote.
ACT
Tanzania inaongozwa na misingi mikuu mitano ifuatayo:-
i)
Uzalendo
ACT-Tanzania
inaamini kwamba kila mwananchi ana wajibu wa msingi kabisa wa kutoa mchango
wake katika jamii na Taifa kwa ajili ya kuhifadhi ustawi wa nchi kwa ajili ya
kizazi cha leo na cha baadaye.
Ili
wananchi waweze kutoa mchango huu kwa dhati na kwa moyo, ni muhimu mazingira
yawepo ya kuhakikisha kwamba wananchi wanaipenda nchi yao. Kwa msingi huu,
ACT-Tanzania itajenga mazingira mwafaka ya wananchi kuipenda nchi yao ili
wajitoe kikamilifu katika kuijenga na kuilinda.
ACT-Tanzania
itajenga mazingira yatakayoongeza uzalendo wa wananchi kwa kuhakikisha uwepo wa
uwazi, ulinzi na utumiaji bora wa rasilimali za taifa na uadilifu wa viongozi.
ACT-Tanzania
inaamini katika usawa katika yyanja zote.
Tunaamini
kwamba mafanikio ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla yatatokana na bidii
katika kazi. Kwahiyo, ACT Tanzania kitapigania kuwepo usawa wa fursa na
mazingira mazuri kwa wote katika kuhakikisha kwamba kila mtu na kila kundi
katika jamii linakuwa na fursa sawa ya kufanya kazi za kujiajiri au kuajiriwa,
na kwamba kipato kitokanacho na kazi halali ndicho kitakuwa kipimo cha mchango
wake katika jamii na taifa.
iii)
Uadilifu.
Uadilifu
katika maisha binafsi na katika jamii utakuwa ndio msingi na mwongozo mkuu wa
viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania. ACT-Tanzania inaamini kwamba uadilifu
ndio msingi na nguzo kuu ya mapambano dhidi ya rushwa na maovu mengine katika
jamii.
iv)
Uwazi na uwajibikaji.
ACT
Tanzania inaamini katika uwazi kwenye mambo yote ya kijamii na kitaifa. Hivyo
basi viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania wana wajibu wa kupigania uwazi
katika mambo yote wanayofanya kwa ajili ya umma.
Sambamba
na uwazi, ACT- Tanzania inaamini kwamba kila mwananchi na kiongozi mwenye
dhamana katika umma ana wajibu katika jamii na Taifa kwa ujumla na ni jukumu
lake kutekeleza wajibu huo bila kinyongo.
Aidha,
mwanachama na kiongozi atokanaye na ACT Tanzania anapaswa kuwajibika kwa maneno
na matendo yake katika utumishi au nje ya utumishi wa chama au taasisi yeyote
ya umma.
ACT
Tanzania inaamini kwamba bidii katika kazi ndiyo njia pekee ya kujipatia
maendeleo.. Hivyo basi wajibu mkuu wa mwanachama wa ACT Tanzania utakuwa ni:-
BIDII KATIKA KAZI.
v)
Demokrasia ya Kweli.
ACT-Tanzania
inaamini demokrasia ndiyo msingi wa kujenga fikra pevu na kueneza uhuru wa mtu,
jamii na Taifa kwa ujumla.
Hivyo
basi, viongozi na wanachama wa ACT-Tanzania watapigania uwepo wa demokrasia ya
kweli katika kila ngazi, ndani na nje ya chama.
Kila
jambo lenye maslahi mapana katika chama na katika umma litaamuliwa kwa njia ya
kidemokrasia ya moja kwa moja au kupitia kwa wawakilishi waliochaguliwa.
4.
Taarifa ya Kazi na mipango ya mbele.
:- ACT
Tanzania imekwisha kukamilisha rasimu ya awali ya Katiba ambaye iliwezesha
kupata usajili wa muda.
:- Zoezi
la kuandikisha wanachama katika mikoa kwa ajili ya kuomba usajili wa kudumu kwa
mujibu wa sheria limekwishakamilika. Tumewapata wanachama katika mikoa yote ya
Tanzania Bara na Zanzibar.
Hata
hivyo, tumechagua mikoa kumi ambayo tungependa msajili akahakiki kama sheria
inavyotaka.
:- Baada
ya kukamilisha zoezi la kuandikisha wanachama, wiki hii kabla ya Ijumaa
tutapeleka fomu na mahitaji mengine husika kwa Msajili wa vyama ili aweze
kupanga ratiba ya zoezi la uhakiki.
:- Mara
baada ya msajili kutoa usajili wa kudumu kwa muda atakaopanga, tutafanya
uchaguzi wa kwanza mkuu.
:- Kama
itampendeza msajili akatupatia usajili wa kudumu mapema, tunatarajia kushiriki
kwa nguvu zote katika chaguzi zote ndogo zitakazojitokeza, uchaguzi wa serikali
za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.
5.
Shukrani.
:- Napenda
kuchukua nafasi hii kuwashukuru waratibu wote wa zoezi zima la uandikishaji
wanachama waliojitolea kwenye mikoa na wilaya mbalimbali katika kuhakikisha
zoezi hili linafanikiwa kwa wakati uliopangwa.
:- Natoa
wito kwa wanachama na wapenzi wa chama popote walipo waendelee kukichangia
chama kwa nguvu zao, muda wao, taaluma zao na kwa kila hali kadri uwezo
unavyomruhsu kila moja wetu.
:- Nawashukuru
sana wataalam na watafiti wetu mbalimbali ambao wamekuwa wakijitolea kutumia
utaalam wao kutushauri katika maeneo mbalimbali ya utafiti, uongozi, sera,
raslimali, usimamizi wa fedha, mawasiliano, sheria, sayansi ya siasa, na
kadhalika.
6.
Wito kwa wanachama na watanzania.
Tunatoa
wito kwa kila mwanachama, mfuasi na mpenzi wa ACT-Tanzania popote walipo nchini
kuhakikisha kwamba:-
:- wanazingatia
misingi ya chama iliyoanishwa hapo juu katika shughuli zao zote. Wakukumbuke
kila mara kwamba lengo kuu la chama hiki ni kupigania na kusimamia mabadiliko
na uwazi katika kila ngazi.
Tungependa
kila shughuli ya chama iwe shirikishi na wazi kwa wanachama na wananchi kwa
ujumla.
:- Anafanya
kazi kwa bidii katika kukijenga chama na kushiriki maendeleo katika jamii
aliyomo,
akizingatia
kwamba chama hiki kinaamini kwamba bidii katika kazi ndiyo njia pekee ya
kujipatia maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Hivyo,
kila mwanachama ahakikishe anatoa mchango wake katika kukijenga chama na kuleta
maendeleo katika jamii husika aliyomo.
:- Tunawakaribisha
watanzania wote popote walipo na wanaoamini katika misingi tuliyoainisha hapo
juu kujiunga na ACT Tanzania.
Kila
mtanzania anayejiunga na chama hiki akumbuke kuchukua wajibu wake katika
kukijenga chama popote pale alipo. Na akumbuke wajibu mkuu kwa mujibu wa chama
hiki kuwa ni:- BIDII KATIKA KAZI.
Mungu
ibariki Tanzania, Mungu ibariki ACT-Tanzania, ahsanteni kwa kunisikiliza!
Kadawi
Lucas Limbu,
Mwenyekiti
wa Taifa
ACT
Tanzania