MAKALA: Je, Unafikiri taarifa ya ukanushi wa account za fb za Mhe. Lowassa zimewavunja moyo mashabiki wake?
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/makala-je-unafikiri-taarifa-ya-ukanushi.html
Katika taarifa kwa umma mapema mwezi february ya ukanushi wa baadhi ya akaunti za mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram na Blogger, Ofisi ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Ngoyai Lowassa ilikanusha kuwa Mhe. Lowassa hamiliki akaunti hizo na hivyo asihusishwe na jambo lolote kuhusiana na taarifa zinazotokana na mitandao hiyo.
Hata hivyo, kwa siku za hivi karibuni, imeonekana kuwa ushabiki wa "Friends of Lowassa" umekua ukipungua siku hadi siku kitu kinachohusishwa na ukanushi huo na ofisi ya Mheshimiwa huyo.
Kiongozi huyo ambae aliwahi Kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anapewa nafasi kubwa ya kunyakua kiti cha Urais wa Tanzania iwapo atagombea nafasi hiyo.
Pamoja na hayo, Mhe. Lowassa amekua Kipenzi wa vijana wengi nchini hasa wale wanaoendesha piki piki za kubeba abiria maarufu kama "BODA BODA" baada ya kufanya vikao vya mara kwa mara vya kuwawezesha vijana hao.
Katika taarifa hiyo pia alisema kuwa anawashukuru watu wote wanao zimiliki akaunti hizo na kudai kwamba wanaonesha penzi yao kwake na analiheshimu hilo.
Baadhi ya Mitandao inayomilikiwa na watu hao ni pamoja na akauti za facebook;
- Friends of Edward Lowassa
- Friends of Edward Ngoyai Lowassa
- Lowassa for 2015
- Dr. Slaa vs Lowassa 2015
Yenye taarifa lukuki kuhusu umoja huo wa Friends of Lowassa.
Imeandikwa na Sebastian Gentanyi | Mhariri Jarida Huru