KIMATAIFA: MUGABE HOI TENA, ARUDI SINGAPORE
http://jaridahuru.blogspot.com/2014/05/kitaifa-mugabe-hoi-tena-arudi-singapore.html
Rais wa Zimbabwe amarejea tena nchini singapore ili kuangalia afya yake kwa mara nyingine. Hii ni miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa jicho huko huko singapore, hii imedhibitishwa na msemaji wake.
George Charamba alisema Mugabe atapitia uchunguzi wa jicho ikiwa ni kulingana na ratiba yake. Rais huyo mwenye umri wa miaka 90 alifanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho katika jicho lake la kushoto mwezi wa pili.
Rais huyo amekuwa na safari za mara kwa mara kuelekea nchini humo ikiwa na baada ya kupigwa marufuku kuenda katika nchi za EU mwaka 2002.
Mugabe, ambaye amekuwa madarakani toka mwaka 1980,alichaguliwa tena kuwa Rais wa nchi hiyo ya Uganda mwezi july mwaka jana katika uchaguzi uliotuhumiwa kuwa na udanganyifu mkubwa na mpinzani wake, waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo, Morrgan Tsvangira.
Safari hizo za mara kwa mara kuenda nchini humo kwa ajili ya matibabu kumewaacha watu wengi na wasi wasi mkubwa juu ya afya ya kiongozi huyo mkongwe.
Moja ya safari iliyozua mijadala mingi ni ile ya mwaka 2012 julai ambayo iliripotiwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na tatizo la Saratani.