jaridahuru

Mitandao

JH STORY: NAOGOPA KU 'CHEAT' NISIJE UMIZWA





1999, Himo - Kilimanjaro
Nilikuwa nimemaliza Chuo Kikuu cha Mlimani wanavyokiita watoto wa siku hizi. Enzi zetu ilikuwa ‘The University of Dar es salaam’ na heshima zote kijijini mtoto wa mangi, Mentor amemalisa sule sote kapisa!! Anyway katika harakati za kutafuta kazi nikawa nafanya kazi kwenye gesti/lodge ya baba pale Himo mjini, kama meneja! Ilikuwa gesti nzuri sana kwa standards za kipindi kile. Kulikuwa na simu kila chumba, feni, choo na bafu ndani na huduma ya bar kwa nje..mahitaji muhimu kwa wale kina infidels.
 
Katika muda niliokaa pale nilipata mikasa na raha nyingi sana. Moja nzuri ninayoikumbuka ni interaction yangu ya kwanza na Polisi. Guest yetu ilikuwa nzuri kiasi cha kwamba wakati ule walipofanya kikao cha Maofisa wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro basi walikodi vyumba na ukumbi katika lodge yetu.
Nakumbuka baada ya kikao chao nilipeleka bill kwa OCS pale Himo kudai malipo ya huduma zote walizopata kwa muda wote wa kikao chao. Alinizungusha sana yule OCS. Siku moja nikaamua kusafiri hadi Moshi Mjini kuonana na RPC nakumbuka enzi hizo alikuwa ni Afande Chiko. Nikaingia moja kwa moja nikamweleza mzee sijalipwa.

Akanyanyua simu akapiga kwa OCS sijui waliongea nini akaniambia nirudi kwa OCS. Kufika kwa OCS namkuta anacheka eti mangi pesa umefuata hadi kwa RPC nikamwambia niliona unanizingua. Akanipa nusu yake akanambia nyingine atanipa baadaye. Kusema kweli hadi leo ile nusu nyingine sijawahi kuipata!!


Hiyo ni topic ya siku nyingine..leo nimekumbuka kisa kilichonifanya nishikilie msimamo wangu wa kutokuoa..at least sio kwa sasa.
 
Unapokuwa gesti unachoangalia ni pesa tu. As long as wateja wanalipa bili wanayofanya humo ndani hayakuhusu..chezea mangi na heleri!!! Siku moja niko ofisini asubuhi mapema, akaja kaka (kwa makadirio ni 28-30yrs) mmoja akakaa kwenye bar pembeni. Mara akae mara asimame..yani he was so restless. Nikamfuata nikamuuliza shida yake.
Mentor: “Habari kaka, sijui nikusaidieje naona umekaa hapa muda bila msaada”
Bro: “Kuna mshkaji namngoja yupo humo ndani chumba namba 28 kuna biashara tunafanya.” Mentor: “Oooh sasa si ungesema kaka, basi ngoja nimpigie halafu nimwambie” Nikamwacha pale nikaenda ofisini na kupiga extension ya chumba namba 28. Akapokea; Mteja (wa chumba namba 28): “Halooo Charles hapa” Mentor: “Hallo ndugu habari za asubuhi” Mteja (Charles ): “nzuri nambie” Mentor: “Kuna ndugu hapa nje anaitwa Robert anasema anakungoja muda mrefu sasa. ” Mara mshkaji akawa kimya ghafla..nikasema nini tena…ikabidi anieleze sasa;
Charles: “dah, menejaee huyo mshkaji wala hatuna biashara naye wala nini. Tafadhali nisaidie niko na mke wake ndani huku atakuwa ametushtukia.”

Kichwa kikagonga..nikashtuka sana nikajua leo msala umeifikia gesti yangu lazima damu imwagike. Sasa Mchaga ninavyopenda pesa mimi (ila mnisamehe tu..ilikuwa enzi zile) ikabidi niwaambie wahudumu wa pale kuwa namwita yule mshkaji, Robert, aje ofisini ili aongee na mteja wangu (wa chumba namba 28 a.k.a Charles). Akiingia tu ndani basi wamtoe yule mkewe wampeleke kwenye nyumba nyingine ya kwetu kama viwanja vitatu mbele.
Basi nikamwita Robert akaingia ofisini, akanyanyua simu. Ile kusikia tu sauti ya Charles akaweka simu chini akashindwa kuongea…akaniambia ndugu Mentor naomba unisaidie. Ikabidi aanze na yeye kunihadithia story yote.
Mkewe aliaga anaenda Kibosho akitokea kwa mjomba wake Tanga. Huku nyuma akasikia kuwa mkewe kaishia Himo kwenye gesti. Nilichompendea huyu jamaa alifanya research yake vizuri hadi chumba walichokuwa wanalala alijua. Akaniomba nimsaidie tu kumpata mke wake amwonyeshe tu kuwa amejua. Ila hakujua huku nyuma mkewe ashatoroshwa.
Nikamwambia siwezi kuwa na uhakika labda twende tukahakikishe chumbani. Tukaongozana wote hadi chumba alimo Charles. Tukagonga akafungua..yani ile kukutanisha macho hata mimi mwenyewe nilijisikia vibaya. Ila kwa kuwa ushahidi ulishaondolewa sikuwa na wasiwasi. Robert akaingia ndani akasachi wee na kweli mkewe hakuwepo. Tukatoka wote nje amechanganyikiwa kabisa.
Haraka haraka Charles akampigia mshkaji wake ambaye kwenye simu alimuita Nelson akaja na mandolini yake. Nakumbuka ilikuwa imejaa maparachichi akamchukua wakaondoka eneo la tukio. Nikamwambia Robert kama vipi akatafute ushahidi zaidi au mkewe yupo sehemu nyingine. Akaondoka, kumbe alienda kituoni Polisi kuripoti kuwa ana uhakika mkewe yupo kwenye gesti yangu na mimi ninamficha.
Huku nyuma ikabidi niwahi home nikamtoroshe yule mke wa Robert. Katika mahojiano ndo akaniambia anaitwa Jasmine na kwamba ni kweli Robert ni mumewe na Charles walikutanaga tu kwenye party ya kazini. Basi nikampakiza kwenye taxi andoke pale.
Wakati narudi gesti nakutana na Polisi mlangoni wakaanza kunihoji kana kwamba wana uhakika 100% ninajua mke wa Robert alipo. Nikakataa...
Wakasema wanafanya ukaguzi vyumba vyote. Wakaanza kukagua wee. Nakumbuka kwenye chumba namba 12 kulikuwa na mteja mwingine kutokea Dar ambaye naye aliniambia yuko pale kwa likizo na kwamba alikuwa na mkewe na wasingependa kusumbuliwa kabisa hata kwa simu. Hivyo polisi walipofika chumba kile nikawaelezea na kuwaomba wakiruke chumba kile na kuendelea na vingine. Robert akang’aka kusema ndo huko mkewe alipo. Niliwaomba sana ila wakakataa ikabidi nimpigie simu kumuomba afungue mlango.
Mentor: “Hallo mteja samahani. Kuna polisi wamekuja hapa wanataka kufanya upekuzi kidogo kuna ndugu anamtafuta mkewe naomba ufungue mlango” Mshkaji akakubali akafungua mlango.
Swali la kwanza kabla hata polisi hawajaanza kumuhoji akamtupia swali Robert, “Unamtafuta mke guest?” Mara akamwita ‘bebii’ wake aje akamwuliza tena, “Huyu ndo mkeo?” Kwa kweli lile swali lilinichoma sana na kujihisi msaliti..
Basi baada ya ukaguzi tukaondoka kuelekea kituoni. Wakamchukua na baamedi mmoja pamoja na mimi na sosoliso hao kwenye PT 0047 ya polisi kituoni Himo. Wakaanza kutuhoji mmoja mmoja...

Zamu yangu ilipofika, Robert aliniuliza swali moja lenye kunifanya nijisikie msaliti hadi leo..
Robert: Mentor, wewe ni dini gani?” Mentor: “Mkriii..mkristo kweli” Robert: “Hivi ndugu yangu kama ungekuwa upo mbele ya padre hapa akakuuliza kama kweli hujui alipo mke wa Robert ungesemaje?”
Mentor: “Hapana, sifahamu alipo!”
Baamedi akaja naye akashindilia msumari wa mwisho kwa kusema kuwa ni kweli aliona mtu akitoka kwa haraka lakini hakujua kama ndo mke wa Robert.
Kwa hali hiyo kesi ikaishia hapo…ila mpaka leo nikikaa nikakumbuka ile siku huwa naogopa sana kuoa.
Wasalaam Wapendwa,
Mentor.


WRITER: MENTOR

Related

Mahusiano 359704446984599118

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item