jaridahuru

Mitandao

MASWALI: MASWALI 10 KWA MBUNGE WA SHINYANGA MJINI - STEVEN MASELE NA MAJIBU YAKE

1.Ditrick Richard, mkazi wa Kata ya Ngokolo.
Kwa kuwa tulikuchagua kuwa mwakilishi wetu na kwa bahati nzuri ukachaguliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini (kabla ya kuhamishwa), kwa nini hujaunganisha umeme katika kata zilizopembezoni kidogo na mjini hata za vijijini?
Jibu: Nashukuru kwa swali zuri Richard. Nikiwa mbunge wa Shinyanga Mjini nashukuru kwa heshima tuliyopewa na Rais kwa kuniteua kuwa Naibu Waziri katika Serikali yake . Bila kujali wizara niliyopo, wajibu wangu ni kusukuma na kuchochea maendeleo katika jimbo langu.
Tuna miradi minne ya kusambaza umeme katika jimbo langu ikiwamo kata za pembezoni za Kizumbi, Ibadakuli, Kolandoto, Old Shinyanga, Ndala, Ndembezi, Mwamalili na Mwawazo. Nimeshawishi wananchi wajenge nyumba bora ili tuwaunganishie umeme, hivyo kazi ya kuunganisha umeme ni endelevu kadri mji unavyokuwa.
2. Dickson Gervas, mkazi wa Shinyanga.
Kwa nini hujawasaidia wachimbaji wadogowadogo wa madini wakatengewa eneo la uchimbaji wa madini badala yake Serikali inaleta wawekezaji wenye leseni kutoka nje na wadogowadogo kunyanyaswa?
Jibu: Kwa kipindi cha miaka mitatu niliyotumika nikiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini kwa pamoja na wenzangu wizarani tumeanza kutenga maeneo mengi kwa wachimbaji wadogo katika maeneo ya Mgusu, Nyarugusu, Lwamgasa kule Geita, Mwabomba, Nyangalata, Mwime kule Shinyanga, Ng’anzo, Biharamulo na Chunya. Pia tumeunda vyama vya wachimbaji wadogo nchini pamoja na shirikisho lao Femata kwa ajili ya kusimamia masilahi yao.
Nimeshughulikia kwa karibu masuala ya wachimbaji wadogo na kupunguza migogoro ya wachimbaji nchini. Pia ni wajibu wangu ulikuwa kuhamasisha uwekezaji mkubwa nchini katika sekta ya madini hivyo siyo kosa pia kushawishi uwekezaji mkubwa.
3. Dickson Gervas, mkazi wa Shinyanga.Umejipangaje kwa Uchaguzi Mkuu maana uchaguzi wa mwaka 2010 ulitangazwa umeshinda kwa kura moja.
Jibu: Kwanza kabisa ieleweke kwamba nilishinda kwa asilimia moja na siyo kura moja. Pili goli ni goli tu kama ni 1-0 ni goli tu cha muhimu ni pointi tatu hata kama goli ni la offside.
Nimejiandaa kushinda kwa kishindo kwa kuwa nimewatendea haki watu wa Shinyanga Mjini, nimeitendea haki nafasi ya ubunge waliyonichagua na bila shaka nimefanya kazi kubwa na kuibadili Shinyanga kuwa mji mzuri wa kisasa.
Nimefanya kazi kubwa kuimarisha huduma za afya, elimu tumejenga maabara na zahanati na kuweka vifaa vya kisasa kwenye hospitali zetu, michezo, vikundi vya ujasiriamali pamoja na usambazaji wa maji na umeme na ujenzi wa barabara. Nimeshughulikia vizuri kero za wananchi.
4. Emma Kamisa, mkazi wa Shinyanga.
Kwa nini kabla ya kwenda kwenye kikao cha Bunge la Katiba hujaonana na sisi wananchi wako ili tukupe ya kwenda kusema huko kwa sababu ulikuwa unatuwakilisha? Lakini umekwenda kuzungumza ya kwako peke yako?
Jibu: Katika wabunge waliowahi kutokea Shinyanga Mjini nashikilia rekodi ya kufanya mikutano mingi ya wananchi. Nina wastani wa mikutano 34 kwa mwaka, maana yake ni mikutano miwili kila kata kati ya kata 17.
Ukweli ni kwamba nafanya vikao vingi na wadau mbalimbali pamoja na kupokea hoja na kero kwa maandishi.
Nitaendelea kufanya mikutano na ofisi yangu ya mbunge imeendelea kuwa wazi saa za kazi za Serikali kama nilivyoahidi na wewe binafsi tumekuwa tukiwasiliana kupitia mitandao ya kijamii, ukurasa angu wa Facebook.
5. Pia uliahidi kata zote utazinunulia matrekta lakini mpaka sasa hakuna kata uliyoinunulia badala yake umewanunulia watu wa Stendi peke yao?
Jibu: Sikuahidi, niliamua baada ya kuwa na matrekta ya mkopo ya Serikali nikasema nitawalipia downpayment kata zote watakapokuwa tayari kulipia sehemu iliyobaki ya deni. Kwa bahati mbaya wahusika katika kata hawakuleta maombi yao kwangu kwa wakati mpaka matrekta yakaisha.
Kwa hiyo nia ilikuwepo lakini sikupata mwamko na ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wahusika hivyo, Stendi kikundi cha vijana wajasiriamali na kikundi kutoka Kata ya Mwamalili walileta maombi kwa wakati na niliwahudumia na kupata matrekta moja moja kila kata.
6. Jackson Godfrey
Kipindi cha kampeni uliahidi utatengeneza barabara za lami kutoka Stendi kwenda Mitumbani na barabara la kuelekea Ndala utaiwekea lami mbona hujatimiza ahadi yako mpaka sasa?
Jibu: Tumepata fedha za mradi wa barabara Manispaa ya Shinyanga kutoka Benki ya Dunia, hivyo barabara hizo na nyingine jumla ya kilomita 30 zitajengwa.
Kumbuka hii ni miradi mikubwa na inahitaji fedha nyingi kutekeleza hivyo inahitaji mipango madhubuti ya kupata fedha na kazi hiyo kwa kushirikiana na madiwani tumeikamilisha na tenda zitatangazwa ili ujenzi ambao utachukua zaidi ya miaka minne uanze. Hivyo ahadi yangu itatekelezwa
7. John Shija wa Kata ya Kambarage.
Wewe ni mbunge wetu tulikuchagua utuwakilishe kupitia CCM, mbona ilani ya uchaguzi uliyoahidi utaitekeleza hujafanya hivyo? Mbona watu wengi wanaoishi pembezoni mwa mji hawana maji wala umeme na hakuna uboreshaji wa shule?
Jibu: Swali lako nimelijibu vizuri kwenye majibu yangu hapo juu. Nimetekeleza ilani na ahadi kwa asilimia 80 mpaka sasa. Nimeboresha usambazaji wa maji na umeme mfano ni Ndala Bondeni na Misufini hawakuwahi kuwa na umeme sasa wanao na maeneo mengine. Ibadakuli, Seseko, Mwamalili na Bushora, kote wamepata maji. Michezo tuna timu ya ligi kuu na elimu nilipochaguliwa hatukuwa na shule ya kidato cha tano na cha sita ya Serikali sasa tunayo, tuna Chuo Kikuu cha Ushirika Kizumbi, ni mengi nimefanya
8. Evarist Kabalo, mkazi wa Kata ya Ngokolo.
Awamu hii ulitoa ahadi kuwa utatuwezesha vijana lakini mpaka sasa hujatuwezesha, kama tutakuchagua tena utaweza au ni propaganda tu zilizozoeleka?
Jibu: Nimetoa mitaji mingi kwa vikundi vya vijana, inawezekana sijaweza kukufikia wewe binafsi, naendelea kusaidia vijana kadri fursa ya kifedha inavyopatikana hivyo tuwasiliane tu. Pia fika ofisi ya mbunge kwa maelezo na utaratibu zaidi.
9.John Mwita, mkazi wa Kata ya Ndala.
Kwa nini shule nyingi zilizopo manispaa hazina madawati na wewe ndiye mwakilishi wetu na wanafunzi kila mwaka wanaambiwa kulipia madawati. Madawati hayo yanapelekwa wapi kila mwaka na wewe kwa nini hufuatilii hilo?
Jibu: Nadhani Mwita utakubaliana nami kwamba katika kipindi changu cha ubunge, nimepunguza kwa kiwango kikubwa michango ya wazazi kuchangia elimu na hayo mambo ya madawati tushirikiane kusimamia hujuma zozote. Nakuahidi nitafuatilia hilo.
10. John Mwita, mkazi wa Kata ya Ndala.
Kwa nini unafadhili timu ya Stand United tu lakini nyingine ndogondogo huzifadhili na wala huzitembelei ambazo ndizo ajira za vijana?
Jibu: Kwanza kumbuka Stand United pia ilikuwa timu ndogo miaka mitatu iliyopita na nimekuwa nikitoa mipira na jezi kwa timu zote za jimbo zima ikiwamo Stand United. Nafurahi kuona kiango cha mpira Shinyanga kinakuwa na kutoa ajira kwa vijana na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Related

politics 2563004712321708723

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item