jaridahuru

Mitandao

ELIMU: CWT YAIPA SERIKALI SIKU 14 KUPANDISHA MSHAHARA, LA SIVYO WALIMU WAPANGA KUANDAMANA NCHI NZIMA


BARAZA la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT), limetoa siku 14 kwa wakurugenzi wa halmshauri nchini kuwapa barua za kuwapandisha vyeo walimu wanaostahili la sivyo watafanya maandamano nchi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema maazimio ya baraza hilo yalifikiwa tarehe 28 mwezi uliyopita mkoani Morogoro.
Mukoba, alisema ifikapo Septemba 15 mwaka huu kama wakurugenzi watakuwa hawajawapatia walimu wanaostahili barua za kuwapandisha vyeo, basi watarajie maandamano ya walimu kwenye ofisi zao.

“Baraza limetoa siku 14 kuanzia siku ya kikao na ifikapo siku ya tarehe 15 kama walimu wanaostahili kupandishwa vyeo watakuwa hawajapewa barua zao, kutafanyika maandano ya nchi nzima kuelekea kwa wakurugenzi wa halmashauri kudai barua hizo, hatupendi hali hii itokee lakini hatufurahishwi na hali ya kutojali haki zetu,” alisema Mukoba.

Aidha, Mukoba alisema Baraza limekemea tabia ya serikali ya kuwanyang’anya walimu madaraja ambayo tayari wamekwishayapokea kwa kisingizio cha kutokuwapo fedha za kulipa.

Alisema hata nyongeza ya mishahara iliyotolewa Julai mwaka huu imepingwa na walimu nchi nzima, kwani mbali ya kuwa ndogo sana imetolewa kwa upendeleo na walimu wanataka kujua ni kwanini watumishi wengine waongezwe kwa asilimia kumi na walimu asilimia 6.35.

Related

Habari Mpya 2137505191816242379

Post a Comment

emo-but-icon

Wadhamini

UJUMBE

JH Katika Facebook

Nyayo zetu twitter

Za Juu

Mitandao

Piga Kura

Je ungependa Tanzania iwe na serikali ngapi?
  
pollcode.com free polls 

ADVERTISEMENTS

Msimamo wa ligi mbalimbali

Football results provided by whatsthescore.com

Mechi Live

Walioko Hewani Kwa Sasa

item